Foundation For Civil Society yaiwezesha CHAVITA PWANI RUZUKU YA MILN 28 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 21 June 2023

Foundation For Civil Society yaiwezesha CHAVITA PWANI RUZUKU YA MILN 28

 



NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA

maipacarusha20@gmail.com


CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Pwani kimepokea sh. Milioni 28 kwa ajili ya kutoa elimu kwa Watendaji Wenyeviti waweze kujumiya kundi hilo kwenye kamati mbalimbali ikiwemo ya afya.


Hayo yamebainishwa na mjumbe wa Chama hicho Tatu Kondo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa semina ambayo inafanyika kwa ufadhili wa Shirika la Foundation For Civil Society.


Amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kutoa elimu, Elimu ya ujumuishwaji kwa watu wenye ulemavu katika vyombo vya watoa maaamuzi.


Kondo amesema elimu hiyo itatolewa kwa kata sita za mradi ikiwemo Mailimoja, Mlandizi, Kongowe, Mtambani, Visiga na Kilangalanga.


Akifungua semina ya siku mbili iliyofanyika mjini Kibaha Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Grace Tete amesema viongozi wanatakiwa kuwatambua wenye ulemavu kwenye maeneo yao.


Tete amesema viongozi wanatakiwa kuwa na takwimu za watu wenye Ulemavu ili miradi ikiibuliwa iwaguse watu wa makundi yote..


Aidha ameelekeza kamati zinazoundwa Watu wenye Ulemavu washirikishwe ili wapate wawakilishi wa kuwasilisha mahitaji yao yapatiwe ufumbuzi.




No comments: