GEF na UNDP YAFADHILI MRADI WA KUPAMBANA NA UJANGILI NA BIASHARA HARAMU YA NYARA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 10 July 2023

GEF na UNDP YAFADHILI MRADI WA KUPAMBANA NA UJANGILI NA BIASHARA HARAMU YA NYARA

 

Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bi. Christine Musisi



Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan Abbas



Na Mwandishi wetu, ARUSHA 


maipacarusha20@gmail.com


 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Julai 10, 2023 akiwa na Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bi. Christine Musisi, ameongoza Kikao cha Kamati Tendaji ya Mradi wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara.

 Mradi huu ni utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara. 


Mradi huu umesaidia sana Serikali katika kukabiliana na ujangili na biashara  haramu ya wanyamapori hususani tembo kwa kuwezesha Doria,  ununuzi wa vifaa yakiwemo magari 10, kutoa mafunzo,  kuwezesha miradi kwa jamii na kuanzisha WMA ya Chamwino


Mradi huo unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa “Global Environmental Facility” (GEF) na UNDP kwa jumla ya USD 6,354,587.


Kikao hicho kimefanyika katika Jengo la Ngorongoro jijini Arusha.

No comments: