MIRERANI WAKUSANYA SHILINGI BILIONI 2.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 10 July 2023

MIRERANI WAKUSANYA SHILINGI BILIONI 2.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

 



Na: Mwandishi wetu, Mirerani


maipacarusha20@gmail.com


AFISA madini mkazi (RMO) wa Mkoa wa kimadini wa Mirerani mhandisi Menard Msengi amesema ofisi hiyo imefanikisha makusanyo ya shilingi 2,611,657,467.20 kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.


RMO mhandisi Msengi ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa yake kwa Waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


RMO mhandisi Msengi amesema makusanyo ya fedha hizo kwa mwaka huo wa fedha ni sawa na asilimia 52.23 ya malengo waliyowekewa.


Ametaja baadhi ya sababu zilizochangia wasifikie malengo ni shughuli za kijiolojia mashapo kuwa katika kina kirefu hivyo migodi mingi kutumia muda mrefu kufanya utanuzi na uwekezaji mdogo.


"Pia ukosefu wa teknolojia za kisasa kwa wachimbaji wadogo, mvua ziliathiri miundombinu ya uchimbaji na usafirishaji madini ujenzi, ukosefu wa miundombinu ya umeme kwenye baadhi ya machimbo ya vito," amesema RMO mhandisi Msengi.


Ametaja mikakati waliyonayo ni kuongeza vituo vya madini ujenzi, kulingana na jiografia ya Wilaya ya Simanjiro, utoaji wa elimu kwa wafanyabiasha wa madini wasio rasmi ili waweze kukata leseni, kufuatilia na kusimamia kwa kina miradi ya ujenzi wa viwanda vya madini ya kinywe.


Amesema ofisi yake Ina wafanyakazi wakudumu 28 na watumishi wa mikataba saba.


Amesema soko la madini linaendelea vizuri na kuna wafanyabiashara wakubwa (Dealers) 27 mpaka sasa na pia ujenzi wa soko litakalotumika kuwahudumia wafanyabiasha wa madini ya Tanzanite unaendelea chini ya shirika la nyumba la Taifa (NHC).


Amesema eneo la kitalu C, kampuni ya Franone Mining and Gems LTD, imefanikiwa kufanya uzalishaji wa kilo 146 za madini ya Tanzanite.


Mhandisi Msengi amesema kiasi hicho cha madini ya Tanzanite kilo 146 kilichozalishwa na kampuni ya Franone Mining LTD kina thamani ya shilingi 709, 574, 190.49 na kuiwezesha Serikali kupata jumla ya shilingi 49,670,193.33.


No comments: