MATUMIZI YASIYO SALAMA YA VIDONGE VYA P2 HUSABABISHA UGUMBA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 28 July 2023

MATUMIZI YASIYO SALAMA YA VIDONGE VYA P2 HUSABABISHA UGUMBA



  


NA: DIANA ELIAS, FJS

maipacarusha20@gmail.com


Wanawake nchini Tanzania wametakiwa kutumia njia salama za uzazi wa mpango na kujiepusha na matumzi ya vidonge vya (P2) vinavyotumika kuzuia Mimba kwani vinaweza kusababisha kutopata mtoto (ugumba) kama vikitumiwa bila ushauri wa madaktari.

 

Akizungumza na maipac media Tanzania, Dk. Daniel Godwin wa maabara ya Usanda iliyopo jijini Arusha jana Julai 27,2023 amesema kuwa matumizi makubwa ya vidonge vya (P2) kwa wanawake huenda ukasababisha ugumba kwa mtoto wa kike vikitumiwa bila uangalifu.

 

Amesema (P2) ni vidonge vinavyo tumika kuzuia Mimba au kuharibu mfumo wa kupata mimba na madhara yake ni pamoja na kuharibu mfumo wa hedhi, kuvuruga homon, kuharibu kuta za uzazi na kusababisha ugumba.

 

 

Dkt. Godwin amewashauri wanawake au wasichana kutumia njia zingine za uzazi wa mpango au kuepuka mimba zisizo tarajiwa ikiwemo kutumia kalenda na mipira ya kiume na kike ili kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa kuliko kutumia vidonge ambavyo madhara yake ni makubwa.

 

Vilevile amewashauri wanawake au wasichana wasizidishe matumizi ya p2 kama njia ya kuzuia mimba zisizo tarajiwa kwasababu dawa hizo zina madhara kwa afya zao.

 

 

Doreen Godfrey (22) mkazi wa kwa mrombo jijini Arusha amesema ajuavyo yeye madhara ya matumiazi ya vidonge vya P2 kwa akina mama ni pamoja na kutokuona siku za hedhi kwa wakati au kwa mpangilio na wakati mwingine kutokuona kabisa siku zao kwa miezi kadhaa.


Kwaupande wake Joyce Isaya (27) mfanyabiashara wa duka la vipodozi maeneo ya kwa mrombo jijini Arusha amesema wanawake wengi Wanatumia p2 bila kujua madhara yake hivyo elimu kuhusu madhara ya vidonge hivi na baadhi ya njia za uzazi wa mpango zingetolewa kwa ukubwa ili wanao tumia njia hizo wajue namna ya kuepuka madhara hayo.

  

 

Sambamba na hayo ameeleza njia zingine ambazo ni salama ili kuepuka mimba zisizo tarajiwa ni kutumia kalenda na mipira ya kiume na kike wakati wa kujamiiana ambayo itazuia mimba pamoja na magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na ukimwi.

 

 

 

No comments: