![]() |
| Salha Ramadhani mkazi wa Mrombo jijini Arusha akizungumza na Maipac Media Tanzania juu ya umuhimu wa kujieleza kwa mtoto wa kike |
![]() |
| Mwanasheria Christina Israel wa ofisi ya mawakili ya Tech. Advocates iliyopo kwa mrombo jijini Arusha akizungumza na Maipac Media Tanzania ofisini kwake mapema leo |
NA: BEATRICE MCHOMVU,
FJS
Wazazi
nchini wametakiwa kuwapa watoto wao haki na uhuru wa kujieleza ili kupunguza
matendo ya Ukatili wanayotendewa na ndugu au jamaa zao majumbani na shuleni.
Uhuru
wa kujieleza kwa mtoto utapelekea wazazi kufahamu madhila wanayokutana nayo
watoto wawapo majumbani na mashuleni na hivyo kupunguza ukiukwaji wa haki za
watoto na hivyo kutengeneza jamii inayoheshimu haki za mtoto.
Christina Israel, mwanasheria kutoka ofisi ya Tech. Advocates amesema hayo leo July 28 ofisini kwake alipokuwa akizungumza na Maipac media Tanzania, kuwa kumpa mtoto haki ya kujieleza sio malezi mabaya na kulingana na sheria ya mwaka 2019 kifungu cha 11 kinasema mtoto ana haki ya kutoa maoni yake.
Amesema kuwa kutompa mtoto haki ya kujieleza ni kosa la jinahi na adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shillingi million 5 au kifungo kisichozidi miezi 6 au vyote kwa pamoja kutokana na kifungu cha 14 cha Sheria za watoto.
Amewashauri wazazi wawape watoto wao nafasi ya kujieleza kwa sababu ni haki kisheria na itawasaidia kujua kama kuna haki zao zimevunjwa au kufanyiwa ukatili na hivyo kuwa rahisi kutatua changamoto zao.
Amesema kuwa uhuru wa kujieleza kwa mtoto yoyote ndiyo msingi thabiti wa kufahamu matendo maovu wanayotendewa watoto na hivyo kupunguza ama kuondoa madhara hayo kwa watoto.
Wilton
Harrison (19) mkazi wa kwa mrombo jijini Arusha anasema anashukuru wazazi wake
walimpa nafasi ya kujieleza toka akiwa mtoto mdogo na hivyo ilikuwa rahisi
kwake kuwaeleza changamoto zozote anazokutana nazo na kutatuliwa na wazazi wake
ila pia imempa nafasi ya kujiamini anaapozungumza mbele ya watu.
Amesema
kuwa ni muhimu watoto kusikilizwa kwa sababu ni haki yao ya msingi toka
kuzaliwa kwao na ndiyo njia pekee ya kusikilisizwa na wanafamilia wengine ili
kutatuliwa changamoto zao.
![]() |
| Mama Safina akiwa dukani kwake amesema haki ya kujieleza kwa mtoto ni muhimu kwa kukuza ufahamu wake |
Kwa
upande wake Mama safina mkazi wa kwa mrombo na mfanyabiashara wa nafaka katika
soko la kwa mrombo, amesema kuwa ni muhimu kuwasikiliza watoto ili kujua
wanachokitaka na kufanyia kazi mawazo yao kwa sababu watoto Wana mawazo makubwa
na mazuri.
Reginald
Mallya (45) mkazi wa Murieti jijini Arusha na Baba wa watoto watatu amesema kwa
upande wake ni muhimu kuwasikiliza na kuwapa watoto uhuru wa kuongea na
kutendea kazi mawazo yao yanaweza kuwa mazuri au mabaya ili wawaelimishe lipi
ni wazo zuri ama wazo baya.
![]() |
| Reginald Mallya mkazi wa Murieti jijini Arusha amesema kuwapa uhuru wa kujiel;eza watoto kunasaidia kupunguza ukatili kwa watoto majumbani |
![]() |
| Wilton Harrison (19) mkazi wa kwa mrombo jijini Arusha anashukuru wazazi wake kwa kumpa uhuru wa kujieleza unaomsaidia sasa kupambana na mazingira ya kazi zake |





No comments:
Post a Comment