Rais Samia afungua kikao cha Bunge la SADC akionesha matumaini kwa vijana - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 3 July 2023

Rais Samia afungua kikao cha Bunge la SADC akionesha matumaini kwa vijana

 

RAIS SAMIA SULUHU HASSANI akifungua kikao Cha 53 Cha jukwaa la mabunge Jumuiya ya Maendeleo mwa Afrika

Spika WA Bunge la jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. Tulia Ackson akizungumza Katika kikao hicho



Mwandishi wetu,Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Rais Samia Suluhu Hassan,Leo amefungua kikao cha 53 cha Jukwaa la Mabunge katika Jumuiya ya Maendeleo mwa Afrika huku akionesha matumaini makubwa ya vijana wakipewa fursa katika kilimo.


Rais Samia katika kikao hicho ameeeleza mikakati ya serikali kuwashirikisha Vijana katika sekta ya Kilimo ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chakula.


Rais Samia amesema Vijana 812 wapo katika vituo 13 vya mafunzo ya Kilimo ambao watapatiwa ardhi baada ya kumaliza mafunzo hayo.


Amesema ili kuwepo na usalama wa chakula katika SADC ni muhimu kushirikisha vijana katika Kilimo.


Amesema Tanzania imeanza mkakati huo ambao unajulikana kama Building better tomorrow (kuwajenga kesho iliyobora)mkakati ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo na kuongeza Mnyororo wa thamani katika mazao ya Kilimo.


Rais Samia amesema, mkakati huo licha ya kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali lakini pia utasaidia kukuza ajira kwa vijana hadi kufikia 1,500,000.


Amesema Tanzania pia imekuwa ikitekeleza kwa kiasi kikubwa Azimio la Maputo la kutenga asilimia 10 ya bajeti katika sekta ya Kilimo ambapo Sasa kiasi kinachotengwa kimefikia zaidi ya Sh 1 trilioni .


"Ongezeko hili la fedha za bajeti katika Kilimo ni kubwa kutengwa ingawa bado haijafika asilimia 10 ya bajeti"amesema


Akizungumzia za SADC amesema bado zinakabiliwa na uhaba wa chakula licha ya kuwa na ardhi kubwa na yenye rutuba.


Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo ni muhimu wabunge kwa kushirikiana na serikali kuongeza ushiriki wa vijana ambao ni wengi kupenda Kilimo.


"Usalama wa chakula katika SADC na suala la ajira kwa vijana ni mambo ambayo yanahitaji mikakati ya pamoja na inawezesha kukabiliana na changamoto hii"amesema


Awali, Rais wa Bunge la SADC,Roger Mancienne amesema wabunge wa SADC katika kikao hicho watajadiliana jinsi ya kuwa na mkakati wa pamoja kukabiliana na suala usalama wa chakula na kuboresha Kilimo ili kujitosheleza kwa chakula.


Amesema pia wabunge watajadiliana kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana lakini pia kutumia fursa zilizopo ili kuongeza ajira na uwekezaji katika sekta ya Kilimo.


Hata hivyo,alipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa na mkakati mzuri wa kuwashirikisha vijana katika sekta ya Kilimo ambao unawezesha pia kukabiliana changamoto ya ajira.


Spika wa Bunge la Tanzania,Dk Tulia Ackson amesema inawezekana nchi za SADC kuondoa tatizo la usalama wa chakula na ajira kwa vijana kama zikishirikiana katika kuendeleza Kilimo .


Amesema nchi za SADC zinauwezo wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chakula bila kutegemea misaada


Dk Tulia amesema kwa Tanzania tayari imeanza kwa kuwatumia vijana katika Kilimo jambo ambalo nchi nyingine zinaweza kujifunza.


"Serikali ya imeweza kuwakusanya vijana na kuwapa elimu ya Kilimo na baadae watapewa bure ardhi ili kuanza kulima kisasa "alisema 


Mkutano huo wa siku Saba ni WA nne kufanyika Tanzania na  unashirikisha wabunge wa SADC kutoka Zimbabwe,Namibia,Sherisheri,Afrika Kusini, Lesotho,Malawi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Eswatini,Angola, Botswana,Zambia, na wenyeji Tanzania.

No comments: