Wabunge SADC,washauriwa kwenda kuona maajabu ya Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 3 July 2023

Wabunge SADC,washauriwa kwenda kuona maajabu ya Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro

 




Mwandishi wetu,Arusha

maipacarusha20@gmail.com


Wizara ya Maliasili na Utalii,imewakaribisha  wabunge nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo nchini na kushuhudia maajabu yaliyopo katika vivutio hivyo.


Wabunge hao wameshauriwa kutorejea katika nchi zao bila kwenda kutalii hifadhi za Tarangire,Manyara, Ngorongoro, Serengeti na Zanzibar.


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya Rais Samia Suluhu kufungua  kikao cha 53 cha Jukwaa la Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) amesema wabunge hao wanafursa ya kuona kilichoelezwa katika filamu ya Royal Tour ambayo iliongozwa na Rais Samia .


Mchengerwa amesema, Tanzania imebahatika kuwa na vivutio vingi vya Utalii ambavyo havipatikani sehemu nyingine yoyote Duniani na ndio sababu idadi ya watalii  imekuwa ikiongezeka.


Amesema mkutano huo ni sehemu pia ya kukuwa sekta ya Utalii ukiwepo Utalii wa mikutano ambao unakuwa kwa kasi hapa nchini.




Hata hivyo, amesema mwezi huu ,Wizara hiyo itatoa taarifa rasmi ya ukuwaji wa sekta ya Utalii na mikakati zaidi ya kukuza sekta hiyo.


Awali Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr Tulia Ackson pia alitoa wito kwa wabunge wa SADC kwenda kutembelea vuvitio vya Utalii.


Amesema wamechagua kikao hicho kufanyika Arusha kutokana na Arusha kuwa lango la Utalii na ni rahisi kutembelea vivutio vya Utalii kama  Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,Manyara, Tarangire na Mlima Kilimanjaro.


Wakizungumzia Tanzania baadhi ya wabunge walieleza kuvutiwa na Ukarimu wa watanzania tangu walipofika nchini.


Rais wa Bunge la SADC Roger Mancienne alisema wamefurahi kufika Tanzania nchi ambayo imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya Utalii.


Amesema Tanzania ina historia kipekee lakini pia ni miongoni mwa nchi zilizoasisi SADC hivyo kuja Tanzania ni faraja kwao.



No comments: