HALMSHAURI YA RUFIJI YAIBUKA MSHINDI WA TATU NANENANE 2023 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 9 August 2023

HALMSHAURI YA RUFIJI YAIBUKA MSHINDI WA TATU NANENANE 2023

 


Na Mwandishi WETU


maipacarusha20@gmail.com


Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imebuka na ushindi wa nafasi ya tatu bora kati ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Pwani zilizoshiriki maonesho ya Nanenane Kanda ya mashariki mwaka 2023.


Akizungumza baada ya kupokea zawadi ya ushindi Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Abdul Chobo amepongeza jitihada za menejimenti kuanzia maandalizi ya maonesho hayo Hadi kufikia tarehe nane Siku ya kilele.


" ushindi huu umetuletea heshima Kubwa kama Halmashauri kwani ushindani ulikuwa mkubwa lakini Kwa namna tulivyojipanga tumeweza kutoka na ushindi."

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Michael Gwimile upande wa kushoto akiwa katika Moja ya mabanda ya halmashauri ya RUFIJI katika maonesho ya nanenane


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji Michael Gwimile ametoa pongezi Kwa Wataalamu na wakulima walioshiriki maonesho Kwa kufanya kazi kama timu na kupelekea kuibuka na ushindi huo.

Maonesho ya nanenane Kanda ya mashariki yalihusisha Mikoa 4 ambayo ni  Mkoa wa Pwani, Dar es salaam, Tanga na Morogoro

No comments: