Mashirika yasiyo ya Serikali nchini yatakiwa kutumia takwimu sahihi kutatua changamoto katika jamii. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 9 August 2023

Mashirika yasiyo ya Serikali nchini yatakiwa kutumia takwimu sahihi kutatua changamoto katika jamii.

 

Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Serikali nchini Tanzania (Tango) Adamson Nsimba akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya kutumia mfumo wa CSO hub jijini Arusha hivi karibuni 


Baraka Kilanga mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano akifundisha namna ya kutumia tovuti ya asasi za kiraia nchini 


Baadhi ya washiriki waafunzo hayo


Na: Andrea Ngobole, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mashirika yasiyo ya Serikali nchini yametakiwa kutumia mfumo wa data katika kufanya maamuzi ya kutatua changamoto katika jamii.


Akizungumza katika warsha ya siku Moja jijini Arusha iliyoandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya Serikali nchini Tanzania (Tango), Mkurugenzi wa Tango Adamson Nsimba, amesema ni vizuri Kila shirika likatumia nguvu kidogo ya takwimu halisi kupata matokeo makubwa katika Miradi wanayotekeleza.


Amesema Tango imeona ni vema kuanzisha kiota atamizi (Portal au Hub) itakayosaidia kutoa taarifa za mashirika yote nchini ili kurahisisha  upatikanaji wa taarifa na maarifa ya kuandika dokezo la mradi, mafanikio ya mradi na kuwezesha jamii kunufaika na Miradi husika kwa kupata taarifa rasmi kupitia tovuti ya asasi.or.tz itakayotoa habari za mashirika yote yaliyojiorodhesha katika tovuti hiyo.


Amesema CSO knowledge hub ni kama supermarket ambapo Kila Moja anaweka taarifa zake katika hub hiyo na kuruhusu Kila Moja kuweza kusoma na kufahamu kwa kina taarifa za shirika husika.

 

Akitoa mada ya namna ya kuweka taarifa katika tovuti hiyo Baraka Kilanga ambaye ndiye ametengeneza hub hiyo amesema uchechemuzi wa kidigiti yaani Digital Advocacy ndiyo njia rahisi zaidi ya kupata takwimu sahihi za namna mradi wa shirika ulivyowafikia wanufaika wa mradi husika.


Amesema taasisi zisizo za serikali zinapaswa kuwa na data sahihi zinazoweza kusaidia kuwa na matarajio ya jambo husika katika jamii husika.


Amesisitiza kuwa na takwimu sahihi kunasaidia kufanya maamuzi sahihi yanayoweza kukubalika na wadhamini wa Miradi kufikia malengo ya taasisi na mdhamini wa mradi.





No comments: