Mahakama Kuu yasimamisha tangazo la pori la Akiba la Pololeti - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 27 August 2023

Mahakama Kuu yasimamisha tangazo la pori la Akiba la Pololeti

 



Mwandishi wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imesimisha kwa muda  tangazo la kulipandisha hadhi pori Tengefu la Paloleti kuwa pori la Tengefu .


Uamuzi huo umetolewa baada ya Wananchi wanane kuomba ruhusa ya mapitio ya Mahakama(   Leave for Judicial Review) juu ya tangazo  la Rais  Samia Suluhu kwenye Gazeti la Serikali GN. NO. 604 ya 2022 iliyotangaza eneo la vijiji 14 vya Loliondo kuwa Pori la Akiba.


Wananchi hao ni, Latang'amwaki Ndwati, Ezekiel Sumare, Kileo Mbirika, Namuru Kitupei, Philemon Ngurumai, Nakoren Taoyia, Metean Sepena na Saitoti Parmwat walikuwa wakipinga tangazo hilo kwani wananchi hawajashirikishwa.


Jaji mahakama Kuu  kanda ya Arusha Devota Kamuzora ndiye ametoa maamuzi hayo ya zuio la muda la tangazo hilo la Rais na ndani ya siku 14 walalamikaji wanapaswa kuwasilisha kesi ya msingi.


Akizungumza kuhusiana na maamuzi hayo, Wakili Denis Oleshangay amesema uamuzi huo wa mahakama Sasa unawezesha wao kuwasilisha kesi ya msingi.


Amesema katika kesi hiyo namba 178 ya mwaka 2022, Wananchi wa vijiji 14 ambavyo vimeathirika baada ya kutangazwa pori hilo wanapinga.


"Wanahoja nyingi lakini miongoni mwa hoja ni wananchi kutoshirikishwa wala Mamlaka ya serikali zao za vijiji jambo ambalo ni kinyume Cha sheria" amesema.


Amesema kutokana na zuio hilo la Mahakama Sasa pori hilo linabaki katika hadhi ya pori tengefu kama ilivyo kuwa awali ilipotangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii.


Amesema hata hivyo wananchi wa Loliondo pia tayari walifungua kesi kupinga tangazo la Waziri wa Maliasili na Utalii ambayo maamuzi yake yatatolewa septemba mosi na Mahakama Kuu.


No comments: