Magunia 237 na kilo 310 za Bangi zachomwa Moto Arumeru - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 19 October 2023

Magunia 237 na kilo 310 za Bangi zachomwa Moto Arumeru

 



Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kamanda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uteketezaji wa magunia ya Bangi


Na Prisca Libaga Maelezo Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Shehena ya  Bangi ikihusisha magunia 237 na kilo 310 za mbegu  imeteketezwa kwa moto kufuatia operesheni iliyofanywa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya (DCEA) kwa  kushirikiana na vyombo vya Ulinzi Usalama katika Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha .


Operesheni hiyo imesimamiwa na Mamlaka hiyo Kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini.


Ni katika operesheni ya kupambana na kilimo na biashara haramu ya  Bangi kilichoshamiri eneo la Kisimiri  wilaya ya Arumeru ambapo Mkuu wa Wilaya hiyo Emmanuela Kaganda amesema lengo ni kubadilisha mtazamo wa wananchi katika kilimo na biashara ya Bangi



Innocent Masangulla ni Mkuu wa Operesheni wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa Mikoa ya Kanda ya kaskazini amesema Operesheni hiyo ni  ya tatu kufanyika Arumeru


Kwa upande wao wananchi wa wilaya ya Arumeru wamesema ni vyema serikali ikaongeza nguvu ya Kupambana na kilimo na biashara ya bangi Arumeru.



No comments: