Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Arusha Loy Thomas Sabaya akizungumza na wajumbe |
Na: Mwandishi Wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Baba mzazi wa Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya Leo amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa Arusha.
Thomas ole Sabaya ameshinda kwa kwa kupata kura 463 kati ya kura 907 zilizopigwa katika nafasi ya Mwenyekiti.
Katika uchaguzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Arusha International Conference Centre ( AICC ) wapinzani wa Mwenyekiti huyo walikuwa ni Dkt Daniel Mrisho Pallangyo aliyepata kura 374 ,Ndugu Solomoni Olesendeka Kivuyo aliyepata kura 59, Ndugu Edna Israel Kivuyo aliyepata kura 10 huku kura 1 ikiwa imeharibika.
Msimamizi wa Uchaguzi huo Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe amepongeza namna ambavyo zoezi hilo la uchaguzi lilivyofanyika kwa utulivu, amani kubwa kutokana hakukuwa na dalili zozote zenye kupelekea vurugu au vitendo vya rushwa

Ushindi wa Sabaya Umechangiwa na kampeni kubwa ambayo ilikuwa inafanywa na Mtoto wake, ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa Arusha.
Lengai ole Sabaya pamoja na makada wengine wa CCM jana na Leo walifanya kampeni nzito kwani awali Sabaya alikuwa hapewi nafasi ya ushindi kutokana na kuwa nje katika siasa kwa muda mrefu.
Hata hivyo wapiga kura kutoka jamii ya Kimasai kutoka Wilaya za Ngorongoro na Longido ndiyo walionekana kuongoza kampeni za kumchagua Sabaya.
Msimamizi wa Uchaguzi huo Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe amepongeza namna ambavyo zoezi hilo la uchaguzi lilivyofanyika kwa utulivu, amani kubwa kutokana hakukuwa na dalili zozote zenye kupelekea vurugu au vitendo vya rushwa
No comments:
Post a Comment