THRDC, THBUB wazungumzia maafa Hanang yalivyogusa Haki za Binaadamu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 7 December 2023

THRDC, THBUB wazungumzia maafa Hanang yalivyogusa Haki za Binaadamu

 

Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu nchini, Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha



Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu akizungumza na waandishi wa Habari 


Na Andrea Ngobole, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora nchini (THBUB) na Mtandao wa watetezi wa haki za Binaadamu (THRDC), wametoa pole kwa Watanzania na wakazi wa Hanang kutokana na maafa ya watu 69 na majeruhi zaidi 100 kutokana na mafuriko.


 Mafuriko ya Tope yameelezwa kugusa Haki za Binaadamu ikiwepo Haki ya Kuishi, haki ya kumiliki mali na Haki nyingine kadhaa za msingi kwa Kila Binaadamu wakiwepo watetezi wa haki za Binaadamu.


Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu na Mratibu wa THRDC, Onesmo Ole Ngurumwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha mapema leo wametoa pole kwa wafiwa wote na kuomba wapone haraka.


Jaji Mstaafu Mwaimu amesema, THBUB inaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa maafa hayo na kuungana na serikali katika hatua ambazo zinaendelea kusaidia waathirika.


Alisema tukio hili linagusa Haki za Binaadamu na wanatoa pole kwa wananchi wa Hanang.


Onesmo Ole Ngurumwa amesema THRDC inashauri serikali na wadau wengine kuwekeza zaidi katika kitengo cha dharura na maafa ili kuwepo na Msaada wa haraka panapotokea maafa.


Amesema Elimu ya maafa inapaswa kutolewa kwa Watanzania wote, kuwepo vitengo imara vya maafa katika halmashauri zote ili kuweza kutoa huduma za haraka inapotokea majanga .


Alisema ni muhimu serikali na wadau kuendelea kuboresha sheria ikiwepo kuundwa Kamati za maafa Kila wilaya na kujengewa uwezo ili kukabiliana na majanga yanapojitokeza.


Mratibu wa Mtandao wa watetezi wa haki za Binadamu nchini, Onesmo Ole Ngurumwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha

No comments: