WALIOSOMA IFM WAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA CHUONI HAPO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 24 December 2023

WALIOSOMA IFM WAKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA CHUONI HAPO

 




Na Mwandishi wetu


maipacarusha20@gmail.com


Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM Alumni) ambao unajumuisha Watumishi na Wanafunzi waliosoma katika chuo hicho na ambao kwa sasa wanafanya kazi maeneo mbalimbali hapa nchini wamekabidhi vifaa vya TEHAMA ikiwemo Projector tatu kwa uongozi wa chuo hicho Jijini Dar es Salaam.


Zoezi hilo limeongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja huo.


Vifaa hivyo Wamekabidhi kwenye hafla iliyoandaliwa na umoja huo na kufanyika katika Ukumbi wa mikutano wa chuo hicho ambapo vifaa hivyo ni sehemu ya michango iliyotokana na Changizo la IFM Alumin Marathon, iliyofanyika tarehe 19 Novemba, 2023 Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Dkt. Yonazi amesema, wamefikia hatua hiyo mara baada ya kuona umuhimu wa kuongeza vitendea kazi kwa uongozi wa chuo hicho ili kuongeza tija katika masuala ya taaluma.


“Tumetoa vifaa hivi kwa lengo la kuendelea kuchochea ufanisi na kusaidia katika kufundisha wanafunzi wanaoendelea na masomo chuoni hapo na kutatua changamoto ya uhaba wa vifaa hivyo, tunaahidi kuendelea kushirikiana kwa kadiri inavyofaa,” alisema Dkt. Yonazi



Naye Mkuu wa Chuo cha IFM Prof. Josephat amemshukuru kwa namna walivyojitoa na kuona umuhimu wa kufanya hivyo na kueleza kuwa, hatua hiyo imewapa furaha na faraja nakupongeza kwa namna walivyojitolea huku akiahidi kutunza na kuvitumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa.


“Vifaa hivi vimekuja wakati sahihi na vitatusaidia sana katika kufundishia wanafunzi wetu, tuendelee kuwashukuru kwa namna mlivyojitoa kwa ajili ya Chuo chetu,” alisema Prof. Josephat




No comments: