EBN Hunting Safari Ltd Watoa Gari Burunge WMA Kupambana na ujangili, Migogoro ya Wanyamapori na Binaadamu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 25 January 2024

EBN Hunting Safari Ltd Watoa Gari Burunge WMA Kupambana na ujangili, Migogoro ya Wanyamapori na Binaadamu

 

Katibu wa EBN Hunting Charles Sylvester kushoto akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo Kadi ya Gari na Gari Aina ya Land cruiser litakalotumiwa na Jumuiya ya Hifadhi Burunge Kudhibiti Ujangili

Meneja Mkuu wa Chemchem Association ambayo inashirikiana na EBN,Clever Zulu akisoma salamu za wakurugenzi wa EBN, Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Viongozi wa Burunge WMA's kabla ya kukabidhi gari hilo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo alizungumza na Viongozi mbalimbali wa Burunge WMA's 


Na: Mwandishi wetu,Babati


maipacarusha20@gmail.com


Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya EBN Hunting Safari Ltd ambayo inafanya shughuli zake katika kitalu cha uwindaji cha Hifadhi ya Jumuiya ya wanyamapori ya Burunge wilayani Babati imetoa gari aina ya Land Cruiser ili kusaidia shughuli za uhifadhi na Kupambana na ujangili katika eneo la Burunge WMA.


Gari hilo ambalo limegharimu shilingi 205 milioni limekabidhiwa na Katibu wa EBN Hunting Safari Ltd , Charles Sylvester kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, Anna Mbogo ambaye nae aliwakabidhi viongozi wa Burunge WMA.


Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Sylvester amesema gari hilo ni sehemu ya makubaliano ya mkataba baina ya EBN na Burunge WMA ambapo baada ya miaka mitano gari jingine jipya litatolewa.


"EBN ina Imani gari hili litatumika vizuri ikiwepo kusaidia kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na Binaadamu lakini pia kukabiliana na ujangili"alisema


Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, Anna Mbogo kwa niaba ya Mkuu ya Mkuu wa wilaya ya Babati, Lazaro Twange aliipongeza Kampuni ya EBN kwa kutekeleza makubaliano ya mkataba kwa wakati.


Alisema gari hilo pamoja na fedha nyingine ambazo zimetokewa na EBN vinapaswa kutumika vizuri kuendeleza uhifadhi na kutatua changamoto za wananchi.


"Vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi hii ya Burunge vimekuwa na Maendeleo makubwa na tunaimani wananchi wataendelea kushiriki katika uhifadhi ili waendelee kunufaika"alisema


Meneja Mkuu wa Chemchem Association ambayo inashirikiana na EBN,Clever Zulu akisoma salamu za wakurugenzi wa EBN, alisema wanaimani kubwa Gari Hilo litasaidia kuimarika uhifadhi katika eneo hilo.


Zulu alisema EBN Hunting Safari Ltd itaendelea kushirikiana na Burunge WMA na wananchi wa Wilaya ya Babati na mkoa wa Manyara katika kuendeleza uhifadhi nakuvutia watalii zaidi.


Mwenyekiti wa Bodi ya Burunge WMA, Patricia William alisema EBN imekuwa na ushirikiano mkubwa katika kuendeleza uhifadhi na Utalii Burunge WMA na wanaimani kuendelea kupata ushirikiano mkubwa.


"Gari hili ni sehemu ya makubaliano yetu na watatupa gari jingine na tunatarajia pia wataendelea kushirikiana na WMA katika kulinda hifadhi hiyo ili kuendeleza Utalii"alisema



Katibu wa Burunge WMA, Benson Mwaise aliahidi kutunzwa kwa gari hilo na kuwa litasaidia sana katika kazi za kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na Binaadamu lakini pia Kupambana na ujangili.



Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Babati Emmanuel Laizer alitaka Burunge WMA kutumia gari hilo kupunguza migogoro ya wanyamapori kuharibu mazao ya wananchi.



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo akimkabidhi Kadi ya Gari Mwenyekiti wa Bodi ya Burunge WMA's Patricia William 



No comments: