MBUNGE OLE LEKAITA AMPONGEZA NA KUMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI KITETO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 4 January 2024

MBUNGE OLE LEKAITA AMPONGEZA NA KUMSHUKURU RAIS SAMIA KWA MIRADI KITETO

 




Na Mwandishi wetu, Kiteto 


maipacarusha20@gmail.com


MBUNGE wa Jimbo la Kiteto Mkoani Manyara, Wakili msomi Edward Kisau Ole Lekaita amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyofanikisha miradi ya maendeleo kwenye jimbo hilo.


Wakili msomi Ole Lekaita ameyasema hayo wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wananchi wa Jimbo la Kiteto na pia kuelezea miradi ya maendeleo kupitia mfuko wa mbunge.



"Ndugu wananchi wenzangu* wa Jimbo la Kiteto nachukua fursa hii kuwatakia Kheri ya Mwaka Mpya 2024*

Namuomba Mwenyezi Mungu awape Baraka, Afya Njema na Neema  katika mwaka huu 2024*.


"Ndugu wananchi wenzangu* baada ya salama za Mwaka Mpya napenda kuwafahamisha kuwa Kamati ya Mfuko wa Jimbo (Mfuko wa Mbunge*) ambayo Mkiti ni Mbunge iliyoketi tarehe 28. 12. 2023* iliweza kujadilia maombi ya miradi ya wananchi kutoka kata Kumi na Mbili (12)* na baada ya kikao kamati ilitenga fedha katika miradi hiyo kwa mchanganuo kama ifuatavyo;


1. Pesa kwaajili ya Umaliziaji wa Vyumba 2 vya Madarasa  Shule ya Msingi Ngarenaro Kata ya Kibaya kiasi cha Shs 5,000,000,*


2. Pesa kwa ajili ya utengenezaji wa madawati Shule ya Msingi Kaloleni Kata ya Kaloleni kiasi cha Shs 5,000,000*


3. Pesa kwa ajili ya Umaliziaji wa Vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Msingi Malimogo Kata ya Lengatei kiasi cha Shs 6,000,000*


4. Pesa kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la Sunya Kata ya Sunya kiasi cha Shs 10,000,000*


5. Pesa kwa ajili ya Utengenezaji Viti na Meza Shule ya Msingi Mbeli Kata ya Partimbo kiasi cha Shs 5,000,000* 


6. Pesa kwa ajili ya Upauzi wa Vyumba 2 Vya Madarasa Shule ya Msingi Osteti Kata ya Chapakazi kiasi cha Shs 6,000,000*


7. Pesa kwa ajili ya Umaliziaji wa Nyumba ya Daktari Zahanati ya Ndaleta Kata Njoro kiasi cha Shs 6,000,000* 

       

8. Pesa kwa ajili ya Utengenezaji wa Madawati Shule ya Msingi Ngabolo Kata Ndedo kiasi cha Shs 5,000,000*     


 9. Pesa kwa ajili ya Ukamilishwaji wa Ujenzi Madarasa 2 Shule Msingi Oloimug'i Kata Namelock kiasi cha Shs 6,000,000*  

 

10. Pesa kwa ajili ya Ukamilishwaji wa Ujenzi Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Kiteto Kata ya Laiseri kiasi cha Shs 6,000,000*                          


 11 . Pesa kwa ajili ya Upauzi wa Nyumba  ya Daktari Zahanati ya Nchinila Kata Dosidosi kiasi cha Shs 6,584,000*           


 12. Pesa kwa ajili ya umaliziaji wa Nyumba ya Waalimu Shule ya Msingi Lembapuli Kata Loolera kiasi cha Shs 5,000,000*                         


"Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa  Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini* kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.*," amesema Wakili msomi Ole Lekaita.


"Ndugu wananchi wenzangu* wa Kiteto tunayo kila sababu ya kutoa shukuran kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa  Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwaajili ya kutatua miradi ya Maendeleo. Tumwombe Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan* Mwenyezi Mungu ampe Afya Njema na kumlinda vyema ili aendelee  na maono yake mazuri katika Kujenga Taifa Letu," amesema.


"Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni," amesema. 


"Ndugu wananchi wenzangu* kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa," amesema Wakili msomi Ole Lekaita.   

 

"MUHIMU:

* Natoa wito kwa watumishi wote na viongozi ngazi za Vijiji na Kata kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati," amesema Wakili msomi Ole Lekaita.

Kiteto yetu inaendelea Kung'ara


Mungu Ibariki Kiteto*! 


Mungu Ibariki Tanzania* !


Mungu ambariki Mhe. Rais wetu Mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments: