Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Mussa Kuji akisaini kitanu cha maombolezo cha kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa nyumbani kwake MONDULI, mkoani Arusha |
Na Mwandishi Wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa), Musa Kuji amesema Lowassa alikuwa kiongozi hodari aliyependa mazingira na uhifadhi Kwa kuendeleza utalii na kuleta maendeleo ya Taifa.
Ameyasema hayo mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo cha kifo cha aliyekuwa waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa nyumbani kwake Monduli mkoani Arusha jana alipofika kutoa pole kwa familia
Amesema Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa wataenzi mema yote aloyoyafanya Lowassa Kwa kuhifadhi na kuendeleza Hifadhi zote za Taifa nchini ili kuongeza chachu ya maendeleo na kuweka mazingira safi Kwa vizazi vijavyo.
Karibu kutazama picha zaidi katika matukio .
No comments:
Post a Comment