MASHIRIKA YA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI YAWATAKA UNESCO KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI WA NGORONGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 10 February 2024

MASHIRIKA YA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NCHINI YAWATAKA UNESCO KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI WA NGORONGORO

 

Odero Charles Odero, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CILAO akisoma tamko mbele ya waandishi wa Habari jijini Arusha 

Na Mwandishi wetu, Arusha


maipacarusha20@gmail.com


MASHIRIKA matano ya utetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania yameiomba tume ya UNESCO kuchukua maoni huru Toka kwa wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro dhidi ya uvunjifu wa Haki za Binadamu katika utekelezaji wa zoezi la uhamishaji wa wakazi hao kwenda Wilayani msomera mkoani Tanga.


MASHIRIKA hayo ya PINGOS forum, Ujamaa Community Resources Team ( UCRT), Civic and Legal Aid Organization (CILAO), Pastoral Women Council (PWC) na shirika la TEST  yametoa tamko Hilo baada ya kuwepo Kwa taarifa ya UNESCO kufanya tathmini Wilayani Ngorongoro na Msomera kuanzia February 3 Hadi February 9 mwaka huu ili kuona kama Kuna uvunjifu wa Haki za Binadamu katika utekelezaji wa zoezi la kuhamisha watu Kwa hiari Toka Wilayani Ngorongoro kwenda Msomera Mkoani Tanga.


Akisoma tamko Hilo Kwa waandishi wa Habari jijini Arusha Odero Charles Odero, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CILAO amesema kuwa tume hiyo haiwezi kupata majibu sahihi kama hawatasikia kauli Toka Kwa wananchi wa kawaida kwani kumekuwa na zuio la kukutanishwa Kwa wananchi na tume hiyo.


Amesema UNESCO walikutana na Serikali Mkoa wa Arusha February 5 pamoja na wizara ya Maliasili na utalii na wadau wengine wa utalii na baadhi ya watu waliohama Kwa hiari lakini haikuweza kukutana na Viongozi wa kisiasa wa kuchaguliwa toka maeneo yao na hivyo kukosa taarifa muhimu zitakazowapa majibu toshelezi dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu.


"Tume hiyo ya UNESCO imeanza shughuli zake Toka February 3 Hadi February 9 itakapomaliza shughuli yake hivyo hofu yetu ni kwamba ikiwa Wananchi wanaolalamika hawatapata nafasi ya kusikilizwa basi majibu yatakuwa si sahihi Kwa tume hiyo" alisema Odero Charles


Amesisitiza kuwa hakuna sababu ya kuzuia wananchi kutoa maoni huru Kwa UNESCO ili kurekebisha pale palipo na kasoro za ukiukwaji wa Haki za Binadamu 

No comments: