MBUNGE LONDO AWATAKA WANANCHI KUFICHUA WATUMISHI WATAKAOTUMIA VIBAYA GARI LA WAGONJWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 12 February 2024

MBUNGE LONDO AWATAKA WANANCHI KUFICHUA WATUMISHI WATAKAOTUMIA VIBAYA GARI LA WAGONJWA

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Mbunge wa Mikumi Denis Londo amewataka wananchi wa kata ya Malolo Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa kutoa taarifa bila woga pindi wanapoona gari ya kubeba wagonjwa (AMBULANCE) likitumika tofauti na malengo yaliyokusudiwa ya kubeba wagonjwa wanaofika kituo cha afya kwa ajili ya kupata hudma ya haraka kwa wagonjwa waliozidi.


Londo ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, amesema hayo katika mkutano na wananachi wa kata hiyo ambapo alikabidhi gari la kubebe wagonjwa kwenye kituo cha afya Malolo.


Amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi kutumia magari ya serikali kama magari yao binafsi na kwenda sehemu za starehe kama baa,ambapo amekemea na kuwaomba wananchi kuwafichua watakapoona  vitendo hivyo.


“Hili si gari la kwenda nalo baa ni gari la kubeba wagonjwa nawakumbusha tu watumishi wa kituo hiki cha afya, wananchi kuweni wakali mtakapoliona gari linatumika vinginevyo toeni taarifa hata kwa kunipigia simu mimi ama kwa viongozi wenu,”amesema.


Aidha amesema lengo la serikali kutoka magari ya kubeba wagonjwa ni katika hali ya kuendelea kuboresha huduma nza afya kwa wananchi.


Baada ya kukabidiwa kwa gari hilo, baadhi ya wananchi walieleza kuwa miaka ya nyuma walikuwa na tatizo la usafiri kwa ajili ya wagonjwa,walikuwa wakilazimika kukodi gari au kubebwa kwenye kitanda kupelekwa Ruaha Mbuyuni na kilichokuwa kikisababisha ni nkutokana na ubovu wa barabara, lakini kwa sasa kupitia mpango wa Mama Samia unaofahamika kama (MMAMA)  na barabara baada ya kutengenezwa gari zilikuwa zikipitika lakini gharama ilikuwa kubwa.


Mkazi wa Kijiji cha Mlaolo Bertha Ngalela amesema baada ya kupatikana kwa gari hilo la wagonjwa kutasaidia wananchi kwani gharama itakuwa ndogo na hata kupungua kwa vifo vyaa wagonjwa waliokuwa wakipoteza maisha njiani ama kukosa fedha.


“Tulikuwa tunatembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya kama kilometa nane kutoka hapa kijijini mpaka barabarani, na matibabu tulikuwa tunaenda kutibiwa Iringa ama mikumi, kwa uwepo wa kituo cha afya na kupatikana gari maisha yatakuwa salama kwetu na hata wagonjwa wanaozidiwa,”amesema.


Mganga mfawidhi wa  kituo cha afya Malolo Dk Yohana Nshashi amesema kabla ya gari la wagonjwa wananchi walikuwa wakipata changamoto kwa kusafiri umbali kupata huduma hasa kwenye hali ya dharura pamoja na wajawazito wanaopata changamoto, upatikanaji wa gari utasadia na kurahisisha utoaji wa huduma kwa akima mama na watu wengine.


“Kupata hili gari ni mwarobaibi au tiba kwa wananchi, na kwa Malolo ni zawadi kubwa kwa kuwa awali haikuwepo,kituo hiki kinahudumia wakazi 13,319 ambao ni kutoka vijiji vine ambavyo ni Malolo A, Malolo B,Chabi na Mbogozi na vijiji vingine vinavyopakana na wilaya ya Kilosa ambavyo ni halmashauri ya Wilaya ya Mpwpwa na Kilolo”amesema Dk Yohana.



No comments: