Viongozi wa Vikoba Burunge WMA watakiwa kuwa mabalozi wa uhifadhi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 12 February 2024

Viongozi wa Vikoba Burunge WMA watakiwa kuwa mabalozi wa uhifadhi

 


Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Babati, Fadhila Nyambulapi ambaye alikuwa mkufunzi katika mafunzo hayo

Katibu Tawala Msaidizi mkoa Manyara, Faraja Ngerageza akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufunga mafunzo Kwa Viongozi wa vikundi 10 vya vicoba


Mwandishi wetu,Babati


maipacarusha20@gmail.com


Viongozi wa vikundi 10 vya kuweka na kukopa(Vikoba) katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge, wametakiwa kuwa mabalozi Wazuri wa uhifadhi ili waendelee kunufaika wa mitaji yenye masharti nafuu ya kuendesha vikundi vyao.



Vikundi 10 vya Vikoba katika eneo hilo vimepewa zaidi ya million 10 na Taasisi ya chem chem association inayofanya shughuli za uhifadhi katika eneo hilo la Burunge   WMA ili viweze kukopeshana na hivyo kujikwamua na umasikini.


Katibu Tawala Msaidizi mkoa Manyara,Faraja Ngerageza akizungumza wakati anafunga mafunzo wa viongozi wa Vikundi 10 vya Vikoba katika eneo la Burunge WMA  alisema viongozi wa Vikoba ambao wamepatiwa mafunzo ya Usimamizi wa Vikoba katika eneo hilo wanapaswa pia kuwa mabalozi wa wahifadhi.



"Mmepatiwa mafunzo ya Usimamizi wa Vikoba na kanuni mpya za serikali sasa kama mnataka kuendelea kunufaika na mitaji katika vikoba vyenu mnapaswa kuwa wahifadhi Wazuri"alisema


Alisema Taasisi ya chemchem imekuwa ikifadhili vikundi hivyo ili pia vichangie kuendeleza uhifadhi,kupiga vita ujangili lakini pia kufanya shughuli za uzalishaji ili kujiongezea vipato.


Awali Meneja wa miradi ya Jamii ya chemchem association, Napendaeli Wazoeli alisema Taasisi hiyo imekuwa inasaidia vikundi hivyo kuweza kukopeshana.


Wazoeli alisema wamewapa ELIMU ili waweze kuendana na sera 2019 ya serikali kuhusu vicoba inayowapa utambuzi BOT na kuwekwa chini ya utawala wa TAMISEMI.


"Taasisi yetu imeweza kuweka vikundi chini ya usimamizi wetu,  wakiendelea kufanya shughuli zao Lakini pia tumekuwa tukiwawezesha ili kuweza kukopeshana"alisema


"Tangu mwaka 2019 tumekuwa tulisaidia vikundi hivi na sasa wameweza kuweka akiba zao na wanakopeshana vizuri"alisema


Alisema licha ya vikundi kupatiwa mafunzo ya kanuni mpya lakini pia vimepewa elimu ya kutunza fedha na wataalam wa NMB Bank  lakini pia vimepewa elimu ya uhifadhi wanyamapori.


Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Babati, Fadhila Nyambulapi alisema viongozi wa vikundi hivyo baada ya mafunzo wanatarajiwa kubadilika na kuendesha Vikoba kisasa.


"Tunatarajia kupungua kesi za watu kukopa fedha na kushindwa kurejesha lakini pia fedha zitatunzwa benki na tunapongeza chem chem kusaidia mafunzo haya"alisema


Viongozi wa vikundi, Bayi Sabida wa kijiji Cha vilima vitatu na Anna Henry Kikundi Cha Isinyai walisema mafunzo hayo yamekuwa na manufaa makubwa kwao.


"Tumejua kutunza fedha, kuandaa taarifa za fedha lakini pia kufanya tathimini  ya utoaji wa mikopo"alisema Anna.


Mafunzo hayo ya siku tatu yalifunguliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati Anna Mbogo na kuhudhuriwa pia ma mmoja wa wakurugenzi wa Chemchem Association Fabia Bausch  ambaye aliahidi kuendelea kuvisaidia vikundi hivyo.



No comments: