MCHENGERWA AWAKARIBISHA WADAU KUSHIRIKI KWENYE SAMIA BOND - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 10 February 2024

MCHENGERWA AWAKARIBISHA WADAU KUSHIRIKI KWENYE SAMIA BOND

 

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa 


Na:Mwandishi wetu MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amezikaribisha taasisi za kifedha hapa nchini kuwekeza kwenye hati fungani ya miundombinu ya ‘SAMIA Bond’ yenye lengo la kuwawezesha wakandarasi wazawa kuongeza mitaji


Pia amefurahishwa na hatua ya Benki ya NMB kuonesha nia ya kuwekeza kwenye hati fungani ya SAMIA Bond


Waziri Mchengerwa ameyasema hayo wakati alipokutana na Uongozi wa juu wa Benki hiyo ofisini kwake Jijini Dodoma


Amesema kuwa maono ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kukuza wakandarasi wazawa ili waweze kupiga hatua na kutekeleza miradi mikubwa ya ndani ya nchi na hata nje ya Taifa letu


“Nchi za wenzetu wamepiga hatua kwenye maeneo mbalimbali na wameendelea kwa kuwezesha wazawa wamewashika mkono wamekua na ndio hao sasa wanakuja mpaka nchini kwetu kutekeleza miradi mikubwa na sisi tunawaamini lakini hii yote ni kutokana na nchi yao kuwekeza kwao kifedha.”


“Ili Taifa letu liweze kupiga hatua lazima tuwekeze kwa wazawa tuna wakandarasi wengi ambao mitaji yao ni midogo na hawana uwezo wa kifedha, hivyo tuwasaidie Watanzania wenzetu,” alisisitiza.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna amesema Benki yao ina uzoefu na uwezo wa kusimamia Hati Fungani ukizingatia hivi karibuni wamekamilisha Jamii Bond ambayo imeleta matokeo makubwa


Amesema kwenye Jamii Bond Benki ilitegemea kukusanya Sh bilioni 100 lakini mpaka muda wa Bond unakamilika benki imefikisha Sh bilioni 212 na iliwezesha kuwavutia wawekezaji wa nje ambao waliwezesha kuleta dola za Marekani nchini kupitia uwekezaji kwenye Jamii Bond.


Tumebaini kuwa imani ya nchi yetu kwa wawekezaji ni kubwa kwa sababu hakuna mtu anaweza kuja kuwekeza kwenye nchi ambayo hawana imani nayo na hii imetushawishi kujenga uwezo wa vijana wetu ndani ya benki, kuweka washauri wa miamala


Hivi karibuni Waziri Mchengerwa aliielekeza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuanzisha mchakato wa upatikanaji wa hati fungani ya miundombinu ya Barabara (TARURA Infrastructure Bond) ya ‘Samia Bond’ kwa kushirikiana na taasisi za kifedha nchini. @nmbtanzania


No comments: