NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KAMISHNA WAKULYAMBA ATINGA KAGERA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 28 February 2024

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KAMISHNA WAKULYAMBA ATINGA KAGERA










Na: Mwandishi wetu, MAIPAC


maipacarusha20@gmail.com


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba amewasili Bukoba Mkoani Kagera, tayari kwa ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa Burigi Wilayani Chato Mkoa wa Geita.

CP Wakulyamba akiwa katika uwanja wa ndenge Bukoba, amepokelewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Ignus Gara, Katibu Tawala Msaidizi, Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Kagera Bw. Isaya Tendega na Maafisa waandamizi wa Uhifadhi.

Katika ziara hiyo pamoja na mambo mengine CP. Wakulyamba atakutana na wananchi katika Mikutano ya vijiji Karagwe, Ngara na Biharamulo, ili kupata uwelewa wa pamoja juu ya Uhifadhi endelevu wa Maliasili kwa Ustawi wa Jamii.  

No comments: