Na Lilian Kasenene,Morogoro
Serikali kupitia Wiara ya Kilimo imewahakikishia wananchi juu ya upatikanaji wa Sukari nchini, huku ikieleza kuwa tayari imeingia shehena ya tani 100,000 ya sukari hiyo ambayo ituzwa kwa bei elekezi y ash 2,700 hadi 3,200 kwa kilo moja.
Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amesema hayo mkoani Morogoro wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Biashara,Viwanda,Kilimo na Mifiugo iliyotembelea viwanda vya Sukari vya MKulazi na Mtibwa ambapo ziara hiyo ilikuwa na nia ya kujionea sababu inayochangia ukosefu wa sukari nchini.
Silinde alikiri kuwepo wa uhaba wa sukari nchin na kwamba umetokana na viwanda kushindwa kualisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kusababisha mafuriko ambayo yamepelekeamashamba kujaa maji na hivyo kusababisha sukari iliyokuwepo kupanda bei.
“Serikali baada ya kuona hilo imechukua hatua kudhibiti changamoto hiyo kwa kuagizza tani hizo laki moja za sukari ambazo zitauzwa kwa bei elekezi ili kumfanya kila mwananchi kuweza kumudu kununua,”amesema.
“Kwa niaba ya Waziri wa Kilimo,tunawahakikishia wananchi kuwepo Kwa unafuu na upatikanaji wa sukari nchini ambayo itapunguza ama kuondooa kabisa tatizo la ukosefu wa sukari,”amesema.
Naibu Waziri huyo amesema Meli tayari zimefika bandarini na zipo kwenye maandalizi ya kushusha mzigo wa sukari ulioagizwa nchini na itauzwa kwa bei hiyo elekezi iliyotolewa na Bodi ya Sukari.
Aidha amesema Serikali kupitia Wizara imeweka mikakati ya muda mrefu na mfupi, ambapo wa muda mrefu ni pmoja na kuondoa kabisa changamoto ya uhaba wa sukari nchini kwa kuongeza uzalishaji katika viwanda vya sukari, huku mkakati wa muda mfupi ukiwa ni kuagiza sukari nje ya nchi hususani katika kipindi ambacho viwanda havizalishi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu ya Bunge Deo Mwanyika amesema kwmba pamoja na kwamba lengo la ziara hilo ni kuangalia changamoto zinazopelekea kushuka kwa uzalishaji wa sukari nchini katika viwanda, amesema wamebaini kuwa changamoto iliyosababishwa na mvua imechangia kwa kiasi kikubwa na kuona kuwa kiwango cha mvua kimeongezeka kwa zaidi ya milimita 720 kutokaa kwenye milimita 200 ya kawaida.
“Tumetembelea mashamba tumeona namna ilivyo vigumu kwa magari kuingia kwenye mashamba na kukata miwa kwa utaratibu wa kawaida,”amesema mwenyekiti huyo.
Aidha ameitaka serikali kuhakikisha inafanikisha zoezi hilo la kuleta sukari nchini ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa urahisi.
Mtedaji mkuu wa kampuni hodhi ya Mkulazi Selestin Some amesema pamoja na changamoto za mvua kuzababisha uzalishaji kusimama, kiwanda katika kipindi cha mik mitano kimekusudia kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 50,000 hadi kufikia tani 75,000.
Aidha Some amesema kampuni imetoa mbegu za miwa kwa wakulima kiasi cha tani 3,223.
Naye mkurugenzi uendeshaji kawanda cha sukari Mtibwa Aberi Mogesi amesema mvua zinazoendelea kunyesha zimeshabaisha miwa kuharibika, barabara kushindwa kupitika kutokana na kusobwa na maji, pamoja na kiwanda kusimamisha uzalishaji.
Mogesi amesema kama kiwanda watahakikisha wanatimiza lengo la kuzalisha tani 70,000, na kwamba kutokana na uwepo wa mvua hizo wamelazimika kuajiri vijana 2000 kwa ajili ya kukata na kubeba miwa.
No comments:
Post a Comment