Mwandishi wetu Babati
Majangili wawili wamekamatwa wakiwa wamewinda Nyama Twiga kwa ajili ya kuuza nyama wilayani Babati mkoa Manyara.
Majangili hao wamekamatwa kutokana na kazi ya Ulinzi wa eneo la Burunge WMA inayofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) askari wa Halmashauri ya Babati, Askari Taasisi ya chem chem ambayo imewekeza katika eneo hilo,Askari wa Burunge WMA na askari wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Kamishna Msaidizi wa mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA),Peter Mbanjoko amesema Watuhumiwa hao, wamekamatwa Jana kutokana na operesheni ya kupambana na ujangili katika eneo hilo.
Amewataja waliokamatwa ni Athuman Issa misanya(23)mkazi wa Mamire na Paul Himid John(23) wilayani Babati mkoa wa Manyara.
"Tumewafikisha polisi na Jumatatu kama taratibu zikikamilika watawafikisha Mahakamani"amesema
Banjoko akizungumzia tukio hilo amewaonya wanaojihusisha na ujangili kwani hawapo Salama.
"TAWA kwa kushirikiana na Polisi na askari wa Burunge WMA chemchem na TANAPA tutaendelea kuimarisha Ulinzi katika eneo la Burunge WMA na mengine na hakuna jangili ambaye atasalimika"amesema
Amesema Watuhumiwa hao ambao tayari wamefikishwa polisi Babati mjini Jana. Wamekamatwa pamoja na vielelezo vyao Nyama ya Twiga ambayo imekutwa katika mifuko, pikipiki moja yenye namba
MC361EDY ambayo ilikuwa imebeba Nyama hiyo.
"Pia Kuna vitu vingine vingi vya ujangili ambavyo tumewakamata navyo "amesema
Mkuu wa Idara ya Ulinzi ya Taasisi ya chem chem ambao wameweza katika eneo Hamis Chamkulu, amesema Watuhumiwa hao walikamatwa Jana saa 12:30 asubuhi.
"Amesema Watuhumiwa hao ni wawindaji haramu na wanatuhumiwa kufanya biashara ya kuuza nyamapori katika Mji wa Babati"amesema
Mwanasheria wa TAWA, Getrude Kariongi amesema katika operesheni hiyo pia mnunuzi mmoja wa jumla wa Nyama ya Twiga ambaye ndiye amekuwa akisambaza mitaani amekamtwa baada ya kutajwa na Watuhumiwa waliokutwa na Nyama.
Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Babati mkoa Manyara, Emmanuel Laizer ametaka wananchi wa wilaya hiyo kutojihusisha na ujangili kwani ni uhujumu uchumi na lazima watakamatwa.
Uwindaji wa Twiga katika eneo hilo imekithiri kutokana na biashara ya magendo ya nyamapori hata hivyo Taasisi ya chem chem kwa kushirikiana na TAWA,Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Burunge WMA wamekuwa na operesheni za mara kwa mara kusaka majangili.
Taasisi ya chem chem association imekuwa ikitoa zaidi ya milioni 450 kila.mwaka Kupambana na ujangili ikiwepo pia kuwezesha mafunzo kwa Askari wa Wanyamapori eneo la Burunge ambayo yamekuwa yakitolewa na TAWA,Jeshi la Polisi Idara ya upelelezi na Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka.
Kamanda wa polisi mkoa Manyara George Katabazi amethitisha kushirikiliwa Watuhumiwa hao.
"Ni kweli wamekamatwa Hawa majangili bado mahojiano yanaendelea"alisem
No comments:
Post a Comment