TANAPA kutumia ndege zisizo na rubani kulinda hifadhi. Yakamata Ng'ombe 261 Burigi-Chato - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 26 February 2024

TANAPA kutumia ndege zisizo na rubani kulinda hifadhi. Yakamata Ng'ombe 261 Burigi-Chato



Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Juma Kuji akizungumza na waandishi wa Habari za uhifadhi nchini 




Mwanasheria wa Hifadhi ya Taifa BURIGI-CHATO Emmanuel Zumba akizungumza na waandishi wa Habari za uhifadhi 

Afisa Uhifadhi Mkuu wa ldara ya Ulinzi, Hifadhi ya Taifa BURIGI-CHATO, Deogratius Mwageni akizungumza na waandishi wa Habari za uhifadhi 




Mussa Juma, MAIPAC

maipacarusha20@gmail.com


Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), limeanza operesheni ya kutumia Tecknolojia za kisasa ikiwepo ndege zisizo na rubani (drone) kudhibiti majangili na wanaoingiza mifugo hifadhini.


Matumizi ya ndege hizo yanatarajiwa kuongeza ufanisi katika Kudhibiti Uhalifu katika hifadhi hasa kutokana na kuweza kufika maeneo mengi ndani ya muda mfupi kuchukuwa picha na kubaini waharibifu maeneo walipo na kutuma ujumbe kwa askari.


Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Juma Kuji akizungumza na waandishi wa habari za Utalii Februari 26,2024 , amesema TANAPA imejipanga kukomesha matukio ya ujangili na uvamizi wa Mifugo hifadhini.


"Tumeanza kutumia Tecknolojia za kisasa kabisa kulinda hifadhi kwa kutumia ndege zisizo na rubani na nyingine lakini pia tunaongeza doria katika hifadhi ili kuhakikisha wahalifu wanakamatwa"amesema


Kamishna Kuji ametoa wito kwa Wananchi kuacha mara moja Tabia za kuingia hifadhini na kufanya uhalifu ikiwepo kuingiza Mifugo kwani lazima watakamatwa .


"Wito wangu kwa wananchi tuendelee kushirikiana kutunza hizi hifadhi kwa faida ya Sasa na vizazi vijavyo,wale ambao wanafanya Uhalifu tuwataje na serikali itaendelea kuchukuwa hatua"amesema


Mifugo zaidi 261 kutoka nchi jirani yakamatwa ndani ya hifadhi


Kutokana na kuimarika kwa Ulinzi katika hifadhi ya Taifa ya Burigi -Chato, Ng'ombe 261 wamekamatwa wakiwa wanachungwa ndani ya hifadhi hiyo.


Akizungumzia tukio hilo,Afisa Uhifadhi Mkuu wa ldara ya Ulinzi,Deogratius Mwageni amesema Ng'ombe hao wamekamatwa eneo la Kimbogo na Miringa katikati ya hifadhi hiyo.


Mwageni amesema kukamatwa kwa Mifugo hiyo ni kutokana na kuimarika Ulinzi na akaonya baadhi ya viongozi wa vijiji kushirikiana na wahalifu kuingiza Mifugo hifadhini.


Mwanasheria na Kitengo cha uchunguzi na kuendeshaji kesi katika hifadhi ya Burigi -Chato, Emmanuel Zumba amesema Mifugo hiyo iliyokamatwa itafikishwa Mahakamani.


"Tumekuwa na operesheni ya kukamata Mifugo hifadhini kuanzia Julai 2024 hadi sasa tumekamata Ng'ombe zaidi ya 1000 na tunakesi 165 na 74 zimetolewa uamuzi na tumeshinda "amesema.


Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Ismail Omar amesema Ulinzi wa hifadhi hiyo sasa umeimarika hali ambayo inasabisha utulivu wa Wanyamapori na Wanyamapori kuanza kuongezeka.


Omar amesema ,changamoto ambayo wanaendelea Kuidhibiti ni kuingizwa Mifugo kutoka nchi jirani na baadhi ya viongozi wa vijiji wasio waadilifu .


"Tuna vijiji 38 vinavyozunguka hifadhi sasa baadhi ya maeneo kuna viongozi wanapokea wafugaji kutoka nchi jirani na kuingiza Mifugo hifadhini hasa katika maeneo ya milima na mabonde"amesema


Hata hivyo, amesema kutokana na matumizi ya Teknolojia za kisasa katika Ulinzi Mifugo imekuwa ikikamatwa na kufikishwa Mahakamani.


"Tunaomba viongozi wachache wa vijiji waache kuhujumu hifadhi na wajuwe lazima tutawakamata wao na Mifugo iliyoingizwa hifadhini"amesema.


Hifadhi ya Burigi -Chato ilianzishwa mwaka 2019 baada ya kupandishwa hadhi na sasa ni miongoni mwa hifadhi bora nchini ambazo Utalii umeanza kuimarika.


No comments: