Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
WATU wawili Juliana Ribart (31)na Mateso Atanas (35)wote wakazi wa wa eneo la Kungwi wamefariki dunia kwa kupigwa Radi katika kijiji cha Kigugu Wilaya ya Mvomero wakati wakiangalia Luninga ndani ya nyumba yao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema hayo wakati akitoa taarifa za matukio mbalimbali kwa vyombo vya habari.
Mkama amesema tukio hilo limetokea Februari 2 mwaka huu saa nane usiku wakati wakiangalia luninga ndani ya nyumba yao katika kijiji hicho cha Kigugu,kata ya Sungaji, Tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero.
Amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mvomero kwaajili ya kusubiri taratibu za mazishi.
Kufutia hali hiyo jeshi la polisi mkoani hapa linatoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari hasa wakati huu wa mvua zikiendelea kunyesha na kusababisha radi.
Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani Morogoro limefanikiwa kuwakamata Yusuph Rashidi (34) bodaboda mkazi wa Ruaha, na Edmond Sengelele (32) mkazi wa Ruaha wakiwa na madumu 19 ya mafuta ya dizeli yenye ujazo lita 20 ambazo jumla ni lita 380 wakiwa wameyabeba kwenye pikipiki .
Amesema baada ya mahojiano ya awali imebainika kuwa ni mafuta hayo wamekuwa wakiyaiba kwenye mradi wa barabara inayojengwa kutokea Kiberege hadi Ifakara.
Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi na watafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika.
No comments:
Post a Comment