MWENYEKITI WA KIJIJI NA WENZAKE WANNE MBARONI KWA KUSAMABAZA TAARIFA ZA UONGO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 24 July 2024

MWENYEKITI WA KIJIJI NA WENZAKE WANNE MBARONI KWA KUSAMABAZA TAARIFA ZA UONGO




Na Mwandishi wetu, KIBAHA

maipacarusha20@gmail.com

JESHI la Polisi mkoa wa Pwani linawashikilia watu wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha kwazoka kwa mahojiano kwa tuhuma za kuzusha na kurekodi kisha kusambaza taarifa za uongo kwenye mitabdao ya kijamii.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo aliyaeleza hayo leo Julai 24 ambapo amesema tukio hilo lilitokea huko Vigwaza kwazoka wilaya ya kipolisi Chalinze watu hao wanadaiwa kujirekodi na kusambaza klipu yao.


Kwa mujibu wa Kamanda watu hao walijirekodi wakieleza kwamba kuna gari aina ya Noah inayopita maeneo mbalimbali kuwateka watoto wadogo huku wakieleza kwamba watoto wawili wa shule ya msingi Vigwaza wameshatekwa.


Amesema Jeshi la Polisi lilifuatilia taarifa hiyo na kubaini kwamba ni ya uongo.


Kamanda Lutumo amewataja watu hao hao kuwa ni pamoja na Aishi Thomas(32), Shomari Zinga(64) Mwenywkiti wa kijiji cha Kwazoka, Alphonce Boniface (54) na Paul Mwanilenzi mwalimu mkuu shule ya Msingi Vigwaza watuhumiwa wrote wakazi wa Kata ya Vigwaza.


Kadhalika Kamanda amesema taarifa hizo zilienea kwa haraka hadi shule ya msingi Mtongani iliyopo Mlandizi na kuleta tahariki kwa wazazi, walimu na watoto wa shule hiyo.


Taarifa hizo pia zilimfikia mmoja wa wazazi Zaituni Shabani ambaye mtoto wake Ismaiya Zuberi (6) alikuwa kati ya waliotajwa kutekwa ili hali kwa wakati huo alikuwa darasani akiendelea na masomo.


Taarifa ya Kamanda huyo ilieleza kwamba baada ya mzazi huyo kupata taarifa aliwafikishia majirani na kuzua taharuki kwa shule hali iliyosababisha kusitishwa masomo kwa wanafunzi wa shule hiyo.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limesema kwa kuzingatia madhara yanayotokana na uzushi wa namna hiyo kuenea kwa haraka halitawafumbia macho watakamatwa na kupitia mchakato wa kisheria na kufikishwa mahakamani.


Mwisho

No comments: