RAIS SAMIA AUNGURUMA NAIROBI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 23 July 2024

RAIS SAMIA AUNGURUMA NAIROBI



Rais Samia akihutubia Mkutano Jijini Nairobi 


Na: Mwandishi Wetu, maipac

maipacarusha20@gmail.com

Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria na kuhutubia Mkutano wa Shirikisho la Maendeleo la Kimataifa (IDA) uliofanyika jijini Nairobi Nchini Kenya mapema leo.
 
Rais Samia katika hotuba yake amesema kuwa Pamoja na miradi mingine, kwa ushirikiano na IDA nchi ya Tanzania  imefanya mambo mengi ikiwemo yafuatayo.

1. Kuboresha eneo la afya ya Mama na mtoto ikiwa ni moja ya mifumo bora zaidi kwa ukanda wa Afrika.

2. Kuimarisha usambazaji umeme vijijini, eneo ambalo pia Tanzania ni moja ya nchi bora zaidi kwenye ukanda huu wa bara la Afrika.

3. Kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, na

4. Kuanza kwa miradi mikubwa ya kudhibiti mafuriko hasa katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo mpango wa uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi ili kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara (Msimbazi Basin Development Project).

Katika hotuba yake hiyo amesisitiza kuwa na sera bora za kifedha toka mashirika ya kimataifa kwa bara la Afrika, zenye masharti na gharama nafuu, zinazotazama kuongeza uwekezaji katika kukuza rasilimali watu na teknolojia na kujikita zaidi katika kukuza uwezo wa kuongeza idadi ya mipango inayotekelezwa kati yake na nchi washiriki.

No comments: