MPDO- LARETO KUWAFUNDA VIKUNDI VYA AKINA MAMA MONDULI USIMAMIZI WA MISITU, UVUNAJI ASALI KUENDELEZA BAIYOANUAI. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 18 July 2024

MPDO- LARETO KUWAFUNDA VIKUNDI VYA AKINA MAMA MONDULI USIMAMIZI WA MISITU, UVUNAJI ASALI KUENDELEZA BAIYOANUAI.



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Isack Joseph akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo taasisi za usimamizi wa misitu kata za Essimingor na Selela wilayani Monduli
Mkurugenzi wa MPDO - LARETO Lebaraka N Laizer akieleza Malengo ya mradi wakati wa uzinduzi bwa mradi huo


Diwani wa Kata ya Selela amewahakikishia ushirikiano MPDO - LARETO wakati wa utekelezaji wa mradi


Na: Andrea Ngobole, maipac



Maipacarusha20@gmail.com



Kamati za mazingira na vikundi vya ufugaji nyuki vya kata za lepurko na selela wilayani Monduli mkoani Arusha vitanufaika na mafunzo ya kujengewa uwezo wa usimamizi wa misitu na uvunaji wa asali na mazao mengine ya nyuki ili kuongeza kipato katika familia.

Kamati hizo zitajengewa uwezo na shirika lisilo la kiserikali la Maasai Pastoralist Development Organization (MPDO– LARETO) katika mradi wa kuwajengea uwezo taasisi zinazohusika na usimamizi wa misitu ya Essimingor na Selela ili kuendeleza baiyoanuai kupitia Mradi wa Mazingira unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kupitia program ya miradi midogo ambayo inasimamiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha, Isack Joseph amezindua mradi huo juzi July 16, mwaka huu katika ukumbi wa Tanzanite uliopo Makuyuni wilayani Monduli mkoani Arusha.

Mwenyekiti Isack Joseph akizungumza katika uzinduzi huo, aliipongeza shirika la MPDO – LARETO kwa kuja na mradi huo ambao ni rafiki kwa utunzaji wa mazingira na pia kunufaisha vikundi vya akina mama, vijana na kamati za mazingira ili kukukza Uchumi wa kaya na jamii kwa ujumla.

"Nawapongeza MPDO – LARETO kwa kuja na mradi huu unaojengea uwezo kamati za mazingira za kata pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa misitu ya Essimingor na Selela ili kuendeleza bayoanuai"alisema mwenyekiti huyo

Mwenyekiti huyo, alisema halmashauri hiyo ipo tayari kushirikiana na MPDO – LARETO Pamoja na asasi za kiraia nyingine zinazo tekeleza miradi katika wilaya hiyo kwani ni sehemu ya maendeleo yanayowafikia wanufaika moja kwa moja.

Amewataka MPDO katika kutekeleza miradi hiyo wahakikishe wanatoa elimu kwa umma dhidi ya athari za ukataji miti na umuhimu wa uhifadhi wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili ili kujilinda dhidi ya ukame unaotokana na ukataji wa miti kuleta atahari za mabadiliko ya Tabianchi.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa MPDO – LATRETO Lebaraka Laizer alisema wanashukuru Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF) kupitia program ya miradi midogo ambayo inasimamiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kwa kuwapatia fedha za kutekeleza mradi huo kwa kata za Selela na Essimingor.

Amevitaja vikundi vitakavyopewa mafunzo hayo kuwa ni inyuata E Maa women group kilichopo kata ya selelal na kukundi ca Nanyori women group Orkisima kilichopo kata ya Essimingor Pamoja na kamati za mazingira zilizopo katika kata hizo.

Baadhi ya wanufaika wa maradi huo waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo Nakaji Melakiti Lukumayi toka kikundi cha Orkisima amelishukuru shirika hilo kwa kuwawezesha katika mradi uliopita ambapo walipewa mashine ya kusaga na mizinga ya nyuki na kuanzisha biashara ndogondogo hivyo wanaamini ujio wa mradi huu utawanufaisha sana kupata mafunzo endelevu ili kukuza mitaji ya kikundi hicho.

Mwenyekiti wa kijijni cha essimingor Lesikali Mollel amesema watatoa ushirikiano mkubwa kwa shirika la MPDO – LARETO katika kutekeleza mradi kwani watu watajua umuhimu wa utunzaji wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa ajili ya Uchumi endelevu.

Naye mwenyekiti wa Kijiji cha selela Longidonyi Lunda, amesema kuwa watatoa ushirikiano wa kila namna kwa mashirika yote yanayotekeleza miradi katika Kijiji hicho ikiwemo MPDO – LARETO ili kurahisisha utendaji wa kazi.


 





No comments: