Ajali yaua wanne vigwaza - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 22 August 2024

Ajali yaua wanne vigwaza





Na Mwandishi wetu , MAIPAC VIGWAZA


maipacarusha20@gmail.com


WATU wanne wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi Kampuni ya Baraka na Lori la Mafuta.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema ajali hiyo imetokea eneo la Vigwaza Halmashauri ya Chalinze wakati basi hilo la abiria lilipokuwa likitokea Dodoma kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.


Lutumo amesema basi hilo liligongana uso kwa uso na Lori la Mafuta lililokuwa likitokea Dar es Salam kuelekea Rwanda na kusababisha vifo vya watu wanne Wanawake kati yao akiwemo mtoto.


Kamanda huyo amesema majeruhi wa ajali hiyo wanaendelea na matibabu katika kituo cha afya Mlandizi.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amefika eneo la tukio ambapo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwa foleni iliyopo wakati jitihada za kuhamisha mafuta kwenye Lori hilo zikiendelea na kulitoa barabarani.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo huku alisema kwamba kwasasa jitihada zinaendelea kuondoa foleni katika eneo hilo na hali kurudi kawaida.


No comments: