HALMASHAURI YA KARATU KUFUNGA CCTV CAMERA ILI KUDHIBITI WATUMISHI WASIOWAAMINIFU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 22 August 2024

HALMASHAURI YA KARATU KUFUNGA CCTV CAMERA ILI KUDHIBITI WATUMISHI WASIOWAAMINIFU

 



NA SOPHIA FUNDI KARATU.


maipacarusha20@gmail.com 


Halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha  imepanga kufunga Camera za ulinzi (CCTV CAMERA) katika maeneo mbalimbali  ya makusanyo ya mapato ndani ya wilaya hiyo lengo likiwa ni kuwadhibiti watumishi wasiowaaminifu.


Madiwani wametoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo 


Akizungumza mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Lucian  katika kikao hicho amesema kuwa kumekuwa na watumishi wasiowaaminifu wa fedha za serikali  katika maeneo ya makusanyo ya mapato ya halmashauri hivyo ni jukumu la halmashauri kuthibiti mapato ya halmashauri.


Madiwani hao kwa pamoja wameridhia Camera hizo kufungwa maeneo ya geti za ukusanyaji wa ushuru,hospitali ya wilaya ,vituo vya afya na baadhi ya zahanati zenye watu wengi lengo likiwa ni kuthibiti fedha za serikali na kuwabaini watumishi ambao siyo waaminifu katika kazi zao.


Wamemwagiza mkurugenzi kuhakikisha zoezi la kununua Camera hizo linakamilika ndani ya mwezi huu na zifungwe  katika maeneo  yote yanayotuingizia mapato halmashauri.


Wamempongeza mkurugenzi na timu yake ya wataalam kwa kazi nzuri wanayofanya ya kukusanya mapato ya Halmashauri hasa kwenye maeneo ya geti za kukusanyia ushuru wa halmashauri.


"Mkurugenzi tunakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya ya kutembelea maeneo ya geti zetu za ushuru bila kujali muda,umekuwa ukitembelea maeneo hayo hata usiku bila kujali,tunakupongeza sana kwa kazi nzuri unayofanya"Amesema Lucian.


"Kuna watumishi ambao siyo waaminifu na kazi zao katika hospitali zetu,vituo vya afya,zahanati, geti za halmashauri na maeneo ya kukusanyia mapato,tembea na halmashauri kwenye Dashbord ya gari ukiwaona watumishi hao kwa kufunga Camera"Amesema Lucian


Akizungumza mkurugenzi wa halmashauri Juma Hokororo amewahakikishia madiwani kutekeleza maazimio yote ya vikao vya madiwani likiwemo la kununua Camera ambapo amewaomba ushirikianao katika kata zao katika kutekeleza miradi mbalimbali.

Mwisho

No comments: