MAIPAC Yazindua Elimu ya Mpiga Kura, Yataka Vijana Kujiandikisha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 4 August 2024

MAIPAC Yazindua Elimu ya Mpiga Kura, Yataka Vijana Kujiandikisha

 

Andrea Ngobole Meneja miradi maipac kushoto, Mussa Juma Mkurugenzi mtendaji wa Maipac katikati pamoja na mtangazaji wa kipindi Cha vijana sunrise radio
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la maipac Mussa Juma akimkabidhi mtangazaji wa kipindi Cha vijana sunrise radio FM ya Arusha kijarida Cha elimu ya mpiga kura mara baada ya kimaliza kipindi

Mussa Juma Mkurugenzi mtendaji wa Maipac akinukuu Sifa za mpiga kura wakati wakizindua elimu ya mpiga kura katika kipindi hicho

 


Na: Mwandishi wetu, Arusha.


maipacarusha20@gmail.com


Taasisi ya Waandishi wa habari ya MAIPAC jana imezindua mradi wa utoaji elimu ya mpiga kura kwa mkoa Arusha na kuwataka vijana waliofikisha. Umri wa miaka 18 na wenye sifa , kwenda kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura.


Wakizungumza katika uzinduzi wa utoaji elimu ya mpiga kura, Mkurugenzi wa MAIPAC,Mussa Juma na Meneja miradi wa Taasisi hiyo, Andrea Ngobole katika kituo cha Radio Sunrise Fm Arusha, walitaka vijana kuanza kujiandaa sasa kujiandikisha katika daftari la Kudumu la wapiga kura.


Juma alisema vijana wenye umri kuanzia miaka 18 wanasifa ya kujiandikisha katika daftari Hilo kama hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi au sheria nyingine zilizotungwa na bunge.


"Vijana mara nyingi wamekuwa wakishiriki katika mikutano ya kisiasa lakini hawajitokezi kujiandikisha kupiga kura na wale waliojiandikisha baadhi Yao wamepoteza vitambulisho Sasa hii ni fursa nyingine kupata haki Yao"alisema


Hata hivyo juma alisema zoezi likianza na kuboresha daftari mkoa Arusha, wanaotaka kujiandikisha au kuboresha taarifa zao haipaswi kutoa taarifa za uongo, na kujiandikisha  zaidi ya mara Moja.


"Lakini pia kuna Tabia ya kuuza ama kununua kadi ya mpiga kura jambo hili halipaswi kufanyika au pia hata kuharibu kadi ya mpiga kura"alisema


Kwa upande wake Ngobole alisema tume huru ya uchaguzi imeandaa vituo vya kutosha vya kujiandikisha au kuboresha taarifa hivyo ni muhimu kujitokeza kwa wingi wakati wa Kujiandikisha kupiga kura.


"Vituo vya kujiandikisha ambavyo tayari vimetangazwa vitafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni hivyo tujitokeze"alisema


Taasisi ya MAIPAC ni miongoni mwa Taasisi ambazo zimepitishwa na tume huru ya Uchaguzi kutoa elimu ya mpiga kura kuanzia mwezi June 2024  Hadi mwezi Machi 2025.


Mwisho

No comments: