RAIS SAMIA AZINDUA BWAWA LA LITA BILIONI 25 MTIBWA SUGAR, AIAGIZA MENEJIMENTI YA KIWANDA KUTUMIA MAAFISA MAZINGIRA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 3 August 2024

RAIS SAMIA AZINDUA BWAWA LA LITA BILIONI 25 MTIBWA SUGAR, AIAGIZA MENEJIMENTI YA KIWANDA KUTUMIA MAAFISA MAZINGIRA

 





Na:Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha Sukari Mtibwa kuhakikisha inawashirikisha maafisa mazingira ngazi ya Taifa katika ujenzi wa mabwawa na kwamba suala la mazingira litiliwe maanani.


Alisema hayo jana katika ziara yake ya siku ya pili mkoani Morogoro, alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Mtibwa na kuzindua bwawa la umwagiliaji na awamu ya tatu ya upanuzi wa mashamba na umwagiliaji wilayani Mvomero .


" Hapa niweke msisitizo, nimeona kazi nzuri mnayofanya ya ujenzi wa mabwawa, tumieni maafisa Mazingira, suala la Mazingira litiliwe maanani, kwenye mabwawa, kiwandani na mashambani" alisema.. 


Rais Samia alisema Serikali yake itaendelea kulinda makundi yote na inapotokea imeegemea upande mmoja wa wanyonge hivyo upande mwingine usione vibaya kwa serikali inasimamia na kutetea maslai ya makundi yote.


Alisema ikitokea sukari imepanda hadi shilingi elfu saba lazima serikali isimame na wananchi kwani ndio walaji na chakula ndio kila kitu.


Alipongeza uongozi wa kiwanda cha Mtibwa kwa kutoa ajira zaidi ya 8,000 kwa vijana na ajira 9,000 kwa wakulima wa nje ambapo upanuzi ukikamilika zitafikia ajira 11,000


Aidha Rais Samia alisema Serikali katika kuthamini wawekezaji imeondoa msamaha wa kodi shilingi bilioni 246 kwa viwanda vitano ambapo kwa kiwanda cha Mtibwa pekee msamaha wa kodi ni shilingi bilioni 80.9.


"Nimeambiwa uwekezaji wa kiwanda cha Mtibwa ni Dola milioni 155 na kwamba upanuzi wake ukikamilika utafikia dola milioni 805, huu sio uwekezaji mdogo, tulizoea kuona uwekezaji kama huu kwa wawekezaji wa nje lakini leo yupo huyu wa ndani,"alisema.


Awali akizungumzia,mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi kiwanda cha Sukari cha Mtibwa Seif Ally Seif alisema wa kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto ya umeme ambapo kati ya pampu 6 zinazopampu maji katika bwawa hilo ni mbili tu zinafanya kazi.


Aidha alimwomba Rais Samia kuwaongezea uwezo wa umeme KVA 132 ambapo kwa sasa zipo 33 ambazo zinashindwa kuendesha pambu zote 6.


Naye Waziri wa kilimo Hussein Bashe licha ya kupongeza kiwanda hicho kwa upanuzi wake alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 650,000 na kwa mwaka huu hali ikiwa nzuri uzalishaji wa sukari utafikia tani 550,000.


Bwawa hilo la Mtibwa la kutengenezwa lina uwezo wa kumebeba Lita bilioni 25.


Katika hatua nyingine,Rais Samia S amezitaka mamlaka za mikoa na wilaya nchini kuhakikisha wanawasimamia vyema wenyeviti wa vijiji ili waache kupokea rushwa ili kuleta suluhu ya migogoro ya ardhi.


Aidha aliwataka viongozi kutumia kampeni mbalimbali za suluhisho la Amani badala ya kutoa matamko.


Alitoa maelekezo hayo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mvomero baada ya kuzindua mradi wa kimkakati wa kuwaunganisha wakulima na wafugaji pamoja uliopewa jina la TUTUNZANE MVOMERO.


Rais alisema kilio kilichopo ni kwamba hawasimamii serikali za vijiji, watu wakishaumizana huko ni rahisi kunyoosha mkono kupokea kuliko kuleta suluhu.


Aliwataka kuwasimamia wenyeviti wa vijiji waache kunyoosha mikono ,na walete suluhu za kweli nacsheria lazima zifuatwe.


Rais Samia pia alimtaka kila Mwananchi kuheshimu Uhuru wa mwenzake kwa kila shughuli anayoifanya ikiwemo ya kilimo na ufugaji kwani wote wanategemeana katika maisha ya kila siku.


Aliwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuwachukulia hatua wale wote watakaoingilia uhuru wa watu kwa manufaa binafsi.


"Kila mmoja aheshimu mipaka ya mwenzie, kama unataka kulisha mifugo kalishe kwenye malisho sio kwenye mashamba, nanyie wakulima muncher kukata mifugo ya wenzenu" alisema.


Rais alionesha kuridhishwa na kampeni hiyo ya kimkakati ya TUTUNZANE MVOMERO na alisema Serikali itausimamia vema huku akiutaka uongozi wa Mkoa na wilaya ya Mvomero pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuusimamia mradi huo wa mfano kwa kutenga bajeti na kuwashirikisha wananchi kikamilifu.


Rais alitumia fulsa ya mkutano wa kuwapatanisha wakulima na wafugaji kwa kuwataka wapeane mikono kama ishara ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.


"Maugomvi mwisho leo na kwamba sasa wote mnakwenda kubadilika na kuingia kwenye mradi mkabadilike mlime mnaolimanna mnaofuga mkafuge, hakuna haja ya kugombana, mtumie mradi huu ,nyie wote mnatupa uhai na mnatupa vitoweo na vyakula" alisema.




Mwisho.

No comments: