THRDC Wasaini Mkataba wa USD 600,000 na WFP Ili Kudumisha Haki za Binadamu Nchini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 4 August 2024

THRDC Wasaini Mkataba wa USD 600,000 na WFP Ili Kudumisha Haki za Binadamu Nchini




Na Mwandishi Wetu, maipac 

maipacarusha20@gmail.com 


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesaini mkataba wa miaka minne wenye thamani ya USD 600,000 na Wellspring Philanthropic Fund (WFP) kwa kipindi cha mwaka 2024-2027.




Mkataba huo mpya umejengwa juu ya muongo mmoja wa ushirikiano wenye mafanikio na WFP, ambapo unalenga kusaidia kwa ujumla kwenye utekelezaji wa Mpango Mkakati wa THRDC wa (2023-2027) wenye malengo mbalimbali ya kudumisha haki za Binadamu.




Malengo makuu ya mpango huo ni pamoja na kuwajengea Uwezo Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, kufanya Shughuli za Uchechemuzi na Ushirikishwaji, kutoa ulinzi kwa Watetezi wa Haki za Binadamu, kuimarisha na Kuendeleza Taasisi




Utekelezaji wa mkataba huo unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 2024 na utaendelea hadi Oktoba 2027,ambapo wanufaika ni Watetezi wa Haki za Binadamu wa Tanzania Bara na Zanzibar.




Kufuatia mashirikiano hayo THRDC imetoa shukrani kwa msaada endelevu wa WFP na kudai kuwa wanayo matumaini kuwa mradi huo utaongeza nguvu zaidi katika kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ya Watetezi wa Haki za Binadamu na kazi ya utetezi wa Haki za Binadamu nchini kwa ujumla.

No comments: