Ole Ngurumwa Ashauri waliozuia Huduma Wananchi Ngorongoro Kuwajibishwa. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 24 August 2024

Ole Ngurumwa Ashauri waliozuia Huduma Wananchi Ngorongoro Kuwajibishwa.



Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binaadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa






Na Mwandishi Wetu


maipacarusha20@gmail.com


Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwaondoa wote waliosababisha kuondolewa huduma za jamii kwa wananchi waishio katika eneo tarafa ya Ngorongoro, kisha aunde tume kufanya uchunguzi ili kufahamu makosa yaliyosababsha kutokea kwa changamoto hiyo na baada ya hapo kukaa na wananchi hao na kujadili namna bora itakayokuwa na manufaa kwa wananchi hao pamoja na taifa kwa ujumla.




Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ujumbe wa Rais Samia kwa wananchi hao kupitia mawaziri William Lukuvi na Palamagamba Kabudi, Olengurumwa amesema kuna haja ya kupatikana kwa suluhu ya kudumu kuepuka migogoro na mizozo kwa Wanangorongoro.




“Ili kuepukana na changamoto hii kabisa kunahitajika kufanyika mambo yafuatayo kwanza watu wote waliosababisha changamoto hizi waliokuwa wanasimamia michakato yote kule Ngorongoro waweze kuondolewa”, ameeleza Olengurumwa na kuongeza,




“serikali ione umuhimu wa kuwa na jamii hii katika jambo lolote watakalotaka kulifanya kuanzia sasa”




Katika hatua nyingine amewapongeza wananchi hao kwa kutetea haki yao na kusimamia misimamo yao bila kufanya vurugu wala kuvunja amani kwa kipindi chote cha maandamano ya takribani siku tano tangu Agosti 18, 2024.

No comments: