Wanahabari watakiwa kuhamasisha ushiriki Mama Samia Legal Aid - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 24 August 2024

Wanahabari watakiwa kuhamasisha ushiriki Mama Samia Legal Aid

 



Na: Mussa Juma,Dodoma

maipacarusha20@gmail.com


Vyombo vya habari nchini vimeombwa kuhamasisha wananchi wajitokeze kupata msaada wa kusheria kupitia kampeni ya Mama Samia Legai Aid ambayo inaendelea nchini.


Hadi sasa Wananchi zaidi ya 493,000 katika Mikoa saba nchini wamepata huduma ya msaada wa kisheria huku kesi za ardhi zikiongoza.


Kaimu Mkurugenzi Huduma za Msaada wa Kisheria  katika wizara ya Katiba na sheria, Ester Msambau akizungumza katika semina ya waandishi wa habari ya kuhusiana na uchaguzi iliyoandaliwa na mtandao aa watetezi wa haki za binaadamu (THRDC) leo jijini Dodoma amesema bado kuna matukio mengi ya ukiukwaji haki za binaadamu ambayo yanapaswa kushughulikiwa kisheria.


"Tunawaomba wanahabari muendelee kuhamasisha wananchi wajitokeze katika maeneo yao kupata msaada wa kisheria"amesema


 amesema,wanatarajia kuanza awamu nyingine ya kutoa msaada wa kisheria  katika mikoa 19 iliyobaki baada ya kufanyika miaka saba.


Amesema,kampeni hiyo imesaidia kutatua migogoro mingi hasa ya mirathi ambayo ilikuwa inaelekea migogoro na wakati mwingine mauaji.


"Tunaomba waandishi muandike habari za kampeini hizi,lakini habari za uchaguzi hasa za jamii iliyoko pembezoni ili waweze kupata taarifa sahihi,"amesema.


Awali Mratibu wa Mtandao wa Watetezi Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa amewaomba waandishi kushirikiana na wasaidizi wa Kisheria katika maeneo yao,kwa kuwa wanasaidia jamii kwa masuala mengi.


Ole Ngurumwa amesema wanahabari wanapaswa kusaidia kampeni ya Mama Samia legal Aid ili watu wajitokeze kwa wingi kupata msaada wa kisheria.


Akizungumzia chaguzi zijazo,Ole Ngurumwa ametaka wanahabari kufanyakazi kwa kuzingatia maadili yao ikiwepo kuandika sawa vyama vyote.


"Kama mkizingatia maadili yetu mtafanya kazi vizuri lakini pia mfike hadi maeneo ya pembezoni"amesema


Awali Mkurugenzi wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini(UTPC), Kenneth Simbaya aliwataka waandishi kujipanga vyema kwa uchaguzi na kuacha kuwa  wapiga kampeni wa wagombea.


"Hatupaswi kuandika habari kwa upendeleo,tuzingatie maadili na sheria za nchi"alisema


Mwanahabari mkongwe,Jesse Kwayu amesema katika chaguzi zilizopita kulikuwa na changamoto nyingi ikiwepo baadhi ya waandishi kuvaa sale za vyama.


"Kama unataka kufanyakazi kwa weledi epuka sana kuwa na upande,tuzingatie maadili licha ya uwepo wa changamoto"amesema.


Mafunzo hayo yameshirikisha baadhi ya wanahabari kutoka mikoa yote nchini ambao wamekuwa wakiandika masuala ya haki za binaadamu na chaguzi.





No comments: