RC SENDIGA AMUAGIZA DC BABATI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 18 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 14 August 2024

RC SENDIGA AMUAGIZA DC BABATI KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 18

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga 


Mwekezaji wa Ardhi hiyo Bi. Anna ofuo ulomi



Na Epifania Magingo, babati


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Babati Mji Lazaro Jacob Twange kuunda kamati ndogo itakayojadili mgogoro wa ardhi  kati ya Wananchi wa Kijiji Cha kiongozi na Anna ofuo ulomi kama mwekezaji mgogoro ambao umedumu kwa Muda wa miaka 18.


Inadaiwa kuwa Anna ofuo ulomi anatambulika kisheria kuwa ni mmiliki Halali wa ardhi kwa eneo la hekari 2 katika Kijiji Cha Kiongozi baada ya kukabidhiwa bila malipo na Wananchi wa eneo hilo kwa hati ya maandishi ya kuwa kama mwekezaji kwa kuwachimbia Wananchi hao kisima Cha maji safi, kukwangua uwanja wa michezo wa Vijana, na kujenga vibanda vya wajasiriamali.


Akizungumza kwenye mkutano maalumu wa Kijiji Cha Kiongozi ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Qeen Sendiga, Mwenyekiti wa kijiji  hicho Thomas Lohay Duwe amesema wanakijiji walikwenda katika eneo la mlima Tlamp na kufanya maandamo wakidai kuwa eneo la ardhi ya Kijiji hicho limezidi kuchukuliwa kwa hekari 10 kinyume na makubaliono ya awali kati ya mwekezaji huyo na Wananchi.


"Huu mgogoro Mi nimeukuta, lakini eneo hili kwa nyaraka tulizokua nazo, ni kweli aliomba hekari  2 kwa barua 2006/2007,na ndani ya hiyo barua kuna msharti alipewa, baada ya makubaliono kati ya yeye na  wanakijiji kwa Muda huo ulipita mda mrefu Hadi 2010, 2014 Wananchi walifanya maandamo kwa maana ya kwamba Wanadai eneo lao linazidi kuchukuliwa kwa Zaidi ya hekari 10.


Amesema, uongozi wa mkoa uliopita ulishugulikia mgogoro huo na kutozaa matunda huku akidai kuwa Anna ofuo ulomi aliamriwa na Serikali hiyo kuvunja majengo yake katika eneo la hekari 2 alizoomba kwa kwakuwa alikiuka masharti ya mkataba na kuonekana pia alifanya uvamizi wa kujimilikisha ardhi ya eneo la mlima huo kinyume na Sheria.


Inaelezwa kuwa wanakijiji wa kiongozi walifanya jitihada za kurudisha eneo  lililovamiwa na mwekezaji huyo na mpaka sasa limeleta manufaa ya kujenga ofisi ya Kijiji  kutokana na mapato yaliyopatikana baada ya eneo  kurudi mikononi mwa Wananchi.


Aidha, Anna ofuo ulomi amekiri kupewa ardhi hiyo huku akitoa sababu ya kutotimiza matakwa ya makubaliano hayo ikiwemo eneo la kuchimba kisima kukosa maji huku akikana tuhuma za kujimilikisha ardhi eneo la mlima Tlamp kinyume na Sheria na kudai kuwa anataka  fidia endapo Sheria ikimtaka kuondolewa katika eneo hilo.


"Mkutano uliitishwa wa kutambulishwa, niliomba eneo hekari 2 pamoja na kutunza mlima uliopo mbele yetu ndivo barua ile ilivojibiwa mwaka 2007 eneo lilipimwa kupitia ofisi ya mkurugenzi ila eneo la mlima halikupimwa kwakua ni Mali ya serikali eneo langu niliendeleza bila mgogoro mpaka 2019 nilipata malalamiko kutoka kwa Wananchi na kuitwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na kunitaka nivunje nyumba ili eneo lirudi Serikali ya kijiji ".


Naye, Mwanasheria wa Mkoa wa Manyara Jackson Kisaka amesema baada ya kufuatilia na kujiridhisha wakabaini kuwa eneo la mlima lilipimwa kinyume na Sheria na kwamba eneo hilo linapaswa kurudi kwa Wananchi kwakua Anna ofuo Ulomi amevunja makubaliono na Wananchi.


"Baada ya kupitia nyaraka mbalimbali na kujiridhisha 

 na kufanya mahojiano ile timu ya wataalamu na Mimi mmoja wapo nikiwepo yulikuja kugundua pia mama amepima na mlima lakini hakuna nyaraka yoyote ile ambayo wanakijiji pia waliridhia kutoa mlima, hivyo upimaji ulikua ni batili na eneo ni Mali ya Wananchi, na eneo la hekari mbili ni Halali kwake ila hakutekeleza matakwa ya Wananchi kwa hiyo imeonekana kwamba mama amevunja makubaliano na Wananchi".


Awali, Qeen Sendiga alikiri kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa Anna ofuo Ulomi ikimtuhumu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Alexandra Mnyeti kumnyang'anya eneo lake na kutaka kurudishiwa ama kupewa fidia.


"Kwa maana nyingine ni kwamba mama Anna aliandika barua ya kunituhumu Mimi mwenyewe kwa kumnyang'anya eneo lake kwakua mimi ndiye mkuu wa mkoa, sasa nimekuja hapa nikiwa mtuhumiwa namba Moja wa mama ana kwamba Kijiji mlimpa eneo na Mimi nikawarudishia".

No comments: