RC SENDIGA AWATAKA WANAFUNZI WA MANYARA GIRLS KUZINGATIA ELIMU ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 14 August 2024

RC SENDIGA AWATAKA WANAFUNZI WA MANYARA GIRLS KUZINGATIA ELIMU ILI WAJIKOMBOE KIUCHUMI

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga kushoto akiwa amevalia  uniform za shule hiyo akisalimiana na Mkuu wa Shule hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga akiwa na wanafuzi wa shule hiyo



Na Epifania Magingo,Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amefanya ziara katika Shule ya Sekondari ya Wasichana  Manyara Girls iliyopo katika kijiji Cha Kiongozi kata ya Maisaka Babati Mjini Mkoani Manyara na kuwavutia wanafunzi na walimu baada ya Kufika Shuleni hapo akiwa amevalia sare za shule hiyo.


Ujenzi wa Shule hiyo umegarimu Shilingi Billion 3 na kuelezwa kuwa kuanzishwa kwa shule hiyo  kumelenga katika kuboresha mazingira rafiki ya ufundishaji hususani kupunguza vikwazo kwa wanafunzi wa kike, kuongeza fursa ya upatikanaji wa Elimu ya Sekondari lakini pia kuhakikisha wanafunzi wote wanaojiunga na Sekondari wanamaliza Elimu hiyo.


Akizungumza na wanafunzi wa Shule hiyo Queen Sendiga amewataka wanafunzi kujituma kwa bidii katika masomo yao pindi wawapo Shuleni hapo na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutatuwa changamoto mbalimbali zilizopo Shuleni hapo ikiwa ni pamoja na kumaliza Ujenzi wa Bwalo la chakula.


"Sasa maelekezo yangu Mimi ni haya sababu sikutegemea kukuta changamoto kwenye risala yenu, Mkurugenzi Cha kwanza ambacho nataka nione mpaka kufika tarehe 30 mwezi huu,ni umaliziaji wa miundombinu ya shule hasa bwalo lile".


Aidha,ametoa msisitizo katika utunzaji wa miundombinu ya shule hiyo ili iweze kudumu miaka mingi na kuwanufaisha wengine.


" Tunategemea hii shule idumu vizazi na vizazi kwasababu ndio alama pekeake na ndio alama ya kwanza kuwepo katika Mkoa huu ambayo bahati nzuri fedha yake imetolewa na Rais wa kwanza mwanamke katika nchi yetu".


Akisoma risala ya shule hiyo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Manyara girls Dakitari Gissela Msoffe amesema kuwa shule hiyo inamatarajio makubwa katika ufundishaji na kutoa wahandasi na madakitari wazuri wanawake bora wenye ujuzi na maarifa katika ushindaji na kutoa huduma sambamba na kutunza miundombinu.




No comments: