Wakazi Ngorongoro, waandamana wafunga barabara, NCAA yawaondoa hofu watalii. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 18 August 2024

Wakazi Ngorongoro, waandamana wafunga barabara, NCAA yawaondoa hofu watalii.

 


Wakazi wa Ngorongoro wakiwa na mabango yanayoainisha changamoto zao


Mwandishi wetu,Ngorongoro


maipacarusha20@gmail.com


Wananchi wakazi wa Tarafa ya Ngorongoro, mkoa wa Arusha, leo wameandamana wakitaka kurejeshewa huduma muhimu na kupinga ukiukwaji wa haki za binaadamu.


Tangu alfajiri wananchi hao walikuwa wamefunga barabara ya Ngorongoro kuelekea hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kusababisha adha kubwa kwa watalii.


Miongoni  mwa madai ya wananchi hao ni ukiukwaji wa haki zao ikiwepo kuwekewa mazingira ya kulazimishwa kuhamia Msomera, kulazimishwa kuingia kwa vibali katika makazi yao, kuhofia kukosa fursa ya kupiga kura baada ya vituo na majina kuhamishiwa Msomera.


Hata hivyo, mapema mchana wa leo Kaimu Meneja uhusiano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Hamis Dambaya alitoa taarifa kuwaondoa hofu watalii.


Dambaya amesema mkusanyiko huo wa wananchi haujazuia kuendelea kwa shughuli na utalii na tayari watalii walikuwa wanatembelea vivutio vya utalii.


Haya hapa ndio maandamano kwa mujibu wa watetezi Tv na tamko la NCAA.



 

No comments: