WAPIGA KURA WAPYA MILIONI TANO KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 25 August 2024

WAPIGA KURA WAPYA MILIONI TANO KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

 





Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Zaidi ya wapiga kura wapya milioni 5 laki 5 na 56 433 wanatarajiwa kujitokeza  katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwenye zoezi la kujiandikisha katika uboreshwaji wa daftari la kudumu la mpiga kura na ambapo kwa mkoa wa Manyara watu laki 1 57 elfu 958  watajiandikisha katika daftari hilo.


Imeelezwa kuwa tume imeweka utaratibu kwa watu wenye ulemavu,wazee,wagonjwa, wajawazito na wakina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao vituoni watapewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni.


Akizungumza katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi Mkoani Manyara Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Jaji Asina.A.Omar amesema kwa yeyote mwenye sifa ya kujiandikisha katika daftari hilo anapaswa kujiandikisha mara Moja tu ili kuepuka uvunjwaji wa Sheria. 


"Mtu yeyote atakayeomba kuandikishwa zaidi ya mara moja atakuwa ametenda kosa la kisheria na akitiwa hatiani adhabu yake ni faini isiyopungua kiasi Cha shilingi laki moja na isiozidi Shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita na kisichozidi miaka miwili au vyote kwa pamoja".


Aidha,Jaji Asina ameviomba vyama vya siasa pia kuwaamini mawakala wao ambao watakuepo vituoni kwaajili ya uboreshwaji wa daftari hilo ili kuepusha uvunjwaji wa Sheria huku akiwataka kuwahamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha.


Naye,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Givness Aswile amesema viongozi wa dini mbalimbali wanawajibu pia kuwahamasisha waumini wao kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha katika daftari hilo kwakua ni haki ya Kila mtanzania mwenye sifa.


Na baadhi ya washiriki wa mkutano huo  akiwemo  Katibu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara  Iddi Mkowa amesema vi vyema Kila chama kifuate utaratibu kwa mujibu wa Sheria na sio kuingilia majuku ya tume ya Uchaguzi  huku Mwakilishi wa wanawake kwa Mkoa wa Manyara Veronica Peter ametoa hamasa wa jamii kushiriki kikamilifu katika uandikishwaji huo.


Zoezi la kujiandikisha uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa mwaka 2024/2025  linabebwa na kauli mbiu isemayo 

"KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA".

No comments: