WATU 34,746,638 WANATARAJIWA KUSAJIRIWA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 25 August 2024

WATU 34,746,638 WANATARAJIWA KUSAJIRIWA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGAKURA.

 


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani




Na Mwandishi Wetu, maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Jumla ya wapiga kura 34,746,638 wanatarajiwa kusajiliwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani mwaka 2025


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhani akielezea maandalizi ya uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura amesema, wanatarajiwa kuongeza wapiga kura wapya 5,586,433.


"Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura 29,754,699 waliopo sasa kwenye daftari baada ya uboreshaji uliofanyika mwaka 2019/2020,"amesema.


Amesema, wapiga kura 4,369,531 wanatakiwa kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.


"Wapiga kura 594,494 wanatarajiwa kuondolewa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye daftari hilo"amesema.


Amesema vituo 40,126 vitatumika kupigia kura baada ya maboresho 2024,vituo 39,709 viko Tanzania bara na 417 viko Zanzibar,"niongezeko la vituo 2,312 ukilinganisha na vituo 37,814 vilivyotumika 2019/2020,"amesema.


"*Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora*"

No comments: