Bodaboda Manyara wahimizwa Kujiandikisha Daftari la mpiga kura - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 29 September 2024

Bodaboda Manyara wahimizwa Kujiandikisha Daftari la mpiga kura

 




Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com


Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara imefanya uhamasishaji kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ikiwa ni maandalizi ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa lengo la kuchagua Viongozi bora.


Imeelezwa kuwa zoezi la uandikishwaji wa daftari la mpiga kura litaanza October 11 hadi 20 huku likiwahitaji wananchi wenye sifa za kujiandikisha kushiriki zoezi hilo kikamilifu kwakua ni haki ya Kila Mtanzania kikatiba.


Uhamasishaji huo umefanyika kwa njia ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji wa Babati ambapo Viongozi wa Halmashauri hiyo wameambatana na kundi kubwa la Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda huku Afisa Utumishi Halmashauri ya Mji wa Babati Gasto Silayo ambae amemuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati amesema lengo la zoazi hilo ni kuhakikisha Kila mwananchi mwenye sifa anashiriki Uchaguzi huo.


"Sifa za mpiga kura lazima awe raia wa Tanzania, lazima awe ametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea,lazima uyo mwananchi awe hajahukumiwa kwenye Yale makosa ya kifo au kifungo Cha mda mrefu, lakini tofauti na hapo wengine wote wanasifa,vilevile kwa mwananchi ambae anataka kugombea lazima awe amefikia umri wa miaka 21 na kuendelea ".


Mwenyekiti wa Maafisa usafirishaji wa pikipiki Mkoani Manyara maarufu kama bodaboda Omar Adam amewataka waendesha pikipiki wote kufikishwa Elimu kwa wananchi katika maeneo Yao wanayofanyia kazi na hata katika mazingira wanayoishi kwakua wao ni mabalozi wakubwa ambao wanakutana na wananchi wengi.


"Sisi tuwe mabalozi katika Mitaa yetu kwasababu mabodaboda wanapita Kila mahali kwaio Leo tumeitwa hapa na Serikali  tumeweza kupewa Elimu tumeweza kupita katika Mitaa mbalimbali kuna watu wameenda huko kiongozi eeh mamire ambako ni Babati Vijijini kwaajili tu ya kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura katika Serikali ya Mtaa".


Aidha,kwa Upande wake Afisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara Bashan Kinyunyu amesema kutakuepo na matukio mbalimbali ikiwemo zoezi la uandikishaji na kufuata zoazi la uteuzi wa wagombea ,kampeni za Uchaguzi pamoja na kufayika Uchaguzi  


Naye Afisa wa Usalama barabarani Wilayani Babati Mkoani Manyara Inspecta Yasin Mdee amewaasa

Madereva bodaboda  kuzingatia Sheria za usalama barabarani nyakati zote wanapokua wanatoa huduma za usafirishaji kwa wananchi.

No comments: