![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Paul Makonda akiwa na madiwani wa Jiji la Arusha waliomaliza muda wao wakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu ujao |
Na Queen Lema, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Paul Makonda amewaomba madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri ya jiji la Arusha kuwa mabalozi wazuri wa kuelezea miradi mikubwa ambayo imetekelezwa na serikali
Aidha endapo watu kama waliokuwa madiwani wataenda Kuelezea kwa wananchi Kwa ufasaha kabisa miradi iliofanyika itaweza kuruhusu wananchi kuendelea kuiamini serikali yao.
Makonda ameyasema hayo Leo wakati akifunga rasmi baraza la madiwani WA jiji la Arusha ambapo pia makonda alitumia mkutano huo kuweza kutoa shukurani kwa madiwani pamoja na aliyekuwa meya WA jiji la Arusha Max Iraqhe.
Alisema ni wakati sahihi sasa wa kuhakikisha kuwa kila aiyekuwa diwani wa baraza Hilo anasemea vyema miradi ikiwa ni pamoja na kusema thamani halisi ya miradi hiyo.
"Tuwe wazalendo na nchi yetu lakini pia tuhakikishe kuwa Yale tulioyaona lakini pia kuyafanya na kupitisha bajeti humu ndani na kisha yakatekelezwa basi tuyaseme tena hadharani kila Mtu aweze kuyajua na kutambua "aliongeza Makonda

No comments:
Post a Comment