Porokwa ateuliwa UN mwakilishi jamii za Asili Afrika - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 21 June 2025

Porokwa ateuliwa UN mwakilishi jamii za Asili Afrika

 


Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Serikali ya wafugaji, wawindaji wa asili na waokota matunda Nchini (Pingo's forum) Wakili Edward Porokwa 


NA: MWANDISHI WETU, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com


Edward Porokwa, Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa mashirika yasiyo ya Serikali ya wafugaji, wawindaji wa asili na waokota matunda Nchini (Pingo's forum) ameteuliwa kuwa mjumbe wa Baraza la umoja wa mataifa wanaoshughulikia haki za Jamii za asili.


 Porokwa, Wakili msomi na mwanaharakati amejipambanua kuwa mtetezi wa haki za watu wa Jamii ya asili kwa miongo miwili Sasa, ataanza kutumikia nafasi hiyo akiwakilisha Tanzania na Bara la Afrika kwa kipindi Cha miaka mitatu kuanzia January 2026.


Uteuzi huo unaifanya Tanzania kwa mara ya kwanza kuwa na mtu wa kuwakilisha Nchi na Bara Zima la Afrika akisaidiana na mjumbe mwingine Toka Nchini Morocco.


Katika uteuzi huo wa wajumbe nane Bara la Afrika imepewa nafasi ya pekee kwa kupewa viti viwili katika jukwaa la kudumu la umoja wa mataifa huku mabara mengine yakiwa na Kiti kimoja Kila moja


 Porokwa amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za Ardhi, uhifadhi wa kitamaduni na mageuzi ya sera ambayo yanazingatia maarifa ya asili na uongozi wa kimila.


 Porokwa anasema kuwa linapokuja suala la Jamii za asili wanachohitaji ni kutambuliwa kwa haki zao na kuheshimiwa kwa Ardhi na Mila za mababu zao.


Jamii za asili ambazo zimepewa hadhi hiyo na Umoja wa Mataifa hapa nchini ni jamii ya Maasai,jamii ya Wahadzabe,Jamii ya Hakie jamii ya Datoga na jamii ndogo ya Hakie.


Mwisho

No comments: