![]() |
| Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan |
![]() |
| Mbunge wa Jimbo la Kusesa, Luhaga Mpina |
NA: Mussa Juma,Meatu
maipacarusha@gmail.com
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezima hoja kadhaa za mbunge wa Jimbo la Kusesa, Luhaga Mpina ikiwepo hoja ya Tembo kuwa kero katika wilaya hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja stendi wilayani Meatu, Rais Samia amesema serikali imekuwa ikichukuwa hatua kudhibiti tembo katika wilaya hiyo.
Amesema vituo vitatu vya askari wa Wanyamapori vya kidhibiti Tembo tayari vimejengwa na vingine vinaendelea kujengwa katika wilaya hiyo.
Hata hivyo, alimtaka Mbunge huyo kufuata tararibu za kutatua changamoto katika jimbo lake ikiwepo kutumia bunge na kufikisha malalamiko kwa Waziri mwenye dhamana.
Alisema Mbunge huyo alipaswa kufuata taratibu kama bado kuna changamoto za Tembo kwa kuwasiliana na Waziri wa Maliasili badala ya kufikisha malalamiko kupitia mkutano huo kwa lengo la kujipatia umaarufu.
Wakizungumza na MAIPAC Media katika mkutano huo baadhi ya wakazi wa Meatu walieleza kudhibitiwa sana matukio ya tembo kuvamia makazi na mashamba tofauti na miaka ya nyuma.
Joram Masunga alisema kuna kambi ya askari wa wanyamapori zimejengwa na mwekezaji katika wilaya hiyo, Mwiba kwa kushirikiana na Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA).
Masunga alisema miongoni mwa vituo hivyo ni kituo kilichojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya uhifadhi ya Friedkin Conservation Fund(FCF) kwa kushirikiana na Kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris kwa gharama ya zaidi ya sh 129.9 milioni katika kijiji cha Ng’hanga kilichopo jirani na pori la akiba la Maswa.
Rehema Masunga alisena vituo vya kudhibiti tembo ambavyo vimejengwa katika wilaya hiyo pia vina nyumba ya askari wa wanyamapori kinahudumia wananchi.
Awali Mbunge Mpina alisema tembo wameongezeka katika wilaya hiyo na kuwa kero kwa wananchi wa Wilaya ya Meatu inayopakana na pori la akiba la Maswa, hifadhi ya jamii ya Wanyamapori ya Makao na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Mwisho.




No comments:
Post a Comment