Na: Queen Lema Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Serikali imeombwa kuboresha mitaala Kwa wanafunzi wenye ulemavu kulingana na aina ya ulemavu walio nao.
Kwa sasa mitaala iliyopo inajumuisha wanafunzi wote wenye ulemavu na mara nyingine unasababisha changamoto kwa watoto wenye aina flani ya ulemavu
Hayo yamesemwa na Bw Gabriel Mhemela ambaye ni makamu Mwalimu mkuu wa shule ya Holly ghost inclusive iliopo Tengeru Wilayani Meru mkoani Arusha wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema mtaaala uliopo ni mzuri sana kwa watoto Ambao hawana ulemavu lakini Kwa wenye ulemavu wakati mwingine huwa unasababisha washindwe kuelewa vyema.
"Mtaala Una mambo mengii sana na maelezo mengi sana sasa unakuta mtoto au mwanafunzi mlemavu ana changamoto nyingine hii inasababisha aelewe Kwa shida Sana wakati angekuwa na mitaala yake wangeelewa haraka Sana"aliongeza.
Wakati huo huo aliwataka hata Wana jamii nao kuhakikisha kuwa wanajifunza lugha za alama Kwa walemavu ili iweze kuwa rahisi kwao kupata mahitaji na misaada hasa wanapohitajika.
"Tunatoa rai Kwa watanzania sasa kuhakikisha kuwa wanajifunza lugha hizi za alama ili Pindi anapotokea mtoto au mlemavu kwenye jamii aweze kupata haki zake za msingi kwani walemavu nao Wana Haki zote za binadamu" aliongeza.
Akiongelea programu maalumu za kuwaongezea ujuzi watoto hasa wenye ulemavu shuleni Hapo alisema kuwa wanapata utaalamu mbalimbali hasa wa stadi za maisha.
"Kwa shule yetu hapa wanajifunza mambo mbalimbali mfano mzuri kuna Ambao wanatusaida kutengeneza mikate wakati wengine wakiwa wanajifunza kushona na hii inawasaidia hata huko mbeleni kuweza kujiajiri.
Alihitimisha kwa kuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanaendelea kushirikiana na shule hiyo ya viziwi ikiwa ni pamoja na kuwapa watoto wote haki ya kupata elimu hasa kwa watoto wenye ulemavu wa kusikia.
Mwisho


No comments:
Post a Comment