Dc Mkude awaahidi Mikopo mafundi Gereji Arusha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 22 October 2025

Dc Mkude awaahidi Mikopo mafundi Gereji Arusha

 




Na Queen Lema,Arusha


maipacarusha@gmail.com 


Mkuu Wa wilaya ya Arusha, Joseph Mkude amewaahidi kuwafanyia utaratibu Wa kupata mkopo yenye riba nafuu Kwa mafundi gereji pamoja na wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika eneo la Mlima Suye jijini Arusha.


Mkude ameyasema hayo Leo jijini Arusha wakati akiongea kwenye mkutano wa hadhara Wa kusikiliza kero kwa wananchi wa kata ya kimandolu pamoja na mafundi Gereji Wa suye


Alisema kuwa kwa sasa Serikali ya awamu ya 6 inapambana sana katika kuhakikisha inawapa nguvu wananchi wake hivyo basi Kwa sasa mara baada ya uchaguzi kupita atahakikisha kuwa wanaohitaji mikopo kutoka Halmashauri ya jiji la Arusha wananufaika.


Alibainisha kuwa kwa upande Wa umoja wa mafundi Gereji  hasa Wa krokoni Arusha wanatakiwa kudumisha umoja wao sanjari na kufuata masharti yote ambayo yanahitajika kisheria Ili waweze kunufaika na mikopo 


"Ndugu mafundi Gereji nimewasikia kuwa mnauhitaji Wa mikopo Ili muweze kujiongeza kwenye kazi zenu nawaahidi Leo naondoka hapa Ila atakuja afisa anayehusika mtakaa pamoja na atawashauri mpite hatua Ipi na Ipi muweze kufikia malengo "Aliongeza Nkude


Wakati huo huo aliwataka wafanyabiashara hasa wa Suye kuhakikisha kuwa wanafuata Sheria Bora za utunzaji Wa mazingira Kwa kuwa mazingira yakiwa mazuri 


Kwa upande wao mwenyekiti umoja wa mafundi Gereji Krokoni Suye,James Agustoni alisema kuwa Mpaka wao kama wataalamu wa ufundi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa Kwa haraka sana 


James alitaja  changamoto hizo kuwa ni pamoja na ubovu wa miundombinu,pamoja na ukosefu Wa hati miliki ya eneo husika ambalo wanalifanyia kazi.


"Sisi Ambao mnatuona hapa tulianzia kazi zetu krokoni tukahamishiwa hapa na mvua zinaponyesha huwa hapa panakuwa pabaya Sana usalama wa maisha yetu yanakuwa hatarini kutokana na mafuriko ambayo yanatokea lami tunaomba Serikali iweze kutusaidia katika suala Hilo"aliongeza"aliongeza


Katika hatua nyingine Mwenyekiti Msaidizi Wa umoja WA mafundi gereji Suye ambaye pia ni mmiliki Wa Nelson Shop, Nelson Natai Alisema kuwa iwapo miundombinu itatengenezwa nakuwa rafiki kwa watumiaji itawawezesha kufanya biashara Kwa uhakika kwani wateja wengi wataweza kufika bila changamoto yoyote.


Nelson alihitimisha kwa kuiomba Serikali kuharakisha maitaji Yao Ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa sana

No comments: