Na Mwandishi Wetu Maipac
maipacarusha20@gmail.com
Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Paul Kimiti, ambaye amehudumu kwenye nafasi mbali mbali za uongozi kuanzia uwaziri na mkuu wa mkoa katika mikoa mbali mbali nchini, chini ya marais watano Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli, amewaasa watanzania wajitokeza kwenda kupiga kura wasidharau hata kidogo, kwa kuwa kupiga kura ni kuchagua ubora wa maisha yao
Aidha kwa tathmini yake amesema Rais Samia atawafaa zaidi watanzania ikiwa watamchagua kwa sababu ameonyesha uwezo mkubwa wa kutekeleza mambo yaliyoleta mabadiliko kwa maisha ya watu ikiwemo ukamilishaji wa miradi mikubwa ya Bwana la Nyerere na SGR.
Hivyo wawe na uhakika kwamba yote aliyoyaahidi atayatekeleza kwa ufanisi zaidi kwa sababu uwezo huo anao, na ameudhihirisha wazi machoni pa watanzania.

No comments:
Post a Comment