
Mkuu Wa wilaya ya Arusha Joseph Mkude
Na Queen Lema Arusha
maipacarusha@gmail.com
Mkuu Wa wilaya ya Arusha Joseph Mkude amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi Arusha Mjini yamekamilika kwa asilimia 100 huku idadi ya vituo vya kupigia Kura ikiongezwa Ili kuraisisha zoezi Hilo.
Mkude amesema hayo Jijini Arusha wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na upigaji wa Kura Hapo kesho kutwa.
Mkude alidai kuwa kwa wananchi Wa Arusha Mjini hawapaswi kuwa na hofu kwa Jambo lolote lile kwa kuwa Amani Ipo pamoja na ulinzi WA kutosha kabisa.
" Tuna mitaa 154 huku vituo vikiwa ni 1051 na tumefanya hivyo Kila mtanzania aweze kupata na kutimiza Haki yake ya kikatiba kusiwe na umbali mrefu sana, na hata Amani Arusha Mjini na yenyewe Ipo tena ya kutosha"aliongeza
Katika hatua nyingine Alisema kuwa ni muimu kwa kila mtanzania kuhakikisha kuwa anakuwa ni sehemu ya Amani na kuachana na vyanzo vyovyote vile ambavyo vinahatarisha amani ya Jamii.
"Siku ya kupiga Kura nawashauri hivi mkishaenda kupiga Kura nendeni nyumbani au sehemu nyingine taratibu alafu jioni sasa msikilize matokeo hii itasaidia kulinda Amani tusiwe na mikusanyiko isiyo na tija"aliongeza.
Alihitimisha kwa kuwataka baadhi ya vijana kuachana na kauli mbaya mbaya dhidi ya Serikali pamoja na tume na badala yake wanatakiwa kujua na kutambua kuwa Amani ni nguzo kubwa sana.
No comments:
Post a Comment