Bolt tanzania Yaongeza idadi ya Ajira nchini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 29 November 2025

Bolt tanzania Yaongeza idadi ya Ajira nchini






Queen Lema Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Mkutano wa wataalamu wa mawasiliano zaidi ya 100 kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umefanyika jijini Arusha na kuibua mijadala mikubwa kuhusu uaminifu kati ya wananchi na taasisi pamoja na nafasi ya sekta binafsi katika kuboresha huduma.


Mkutano huo unaojulikana kama East Africa PR Week umehusisha maofisa uhusiano kutoka sekta mbalimbali huku kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt ikivuta hisia za wengi kutokana na mchango wake katika kuleta ajira na kuchochea uchumi wa Tanzania.

Akizungumza kwenye mkutano huo Meneja mahusiano ya umma kampani ya kimataifa ya usafiri bolt Tanzania Gilbert Ginono amesema imekuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi nchini na imewafungulia vijana wengi milango na kutoa fursa za kujipatia kipato kupitia shughuli za uendeshaji na usafiri wa mtandaoni


Amesema vijana wengi sasa wanategemea Bolt kupata kipato cha kila siku na kwamba mfumo huo wa kidigitali umeongeza mzunguko wa fedha na kutoa matumaini kwa wanaotafuta ajira mijini.


Ginono amesema pia kuwa Bolt imekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wanaotaka kuingia kwenye sekta ya usafiri ambapo idadi yao imeongezeka kwa kasi katika miaka ya karibuni.


Ameeleza kuwa uwepo wa wanawake kwenye mfumo wa Bolt umeongeza usawa wa kiuchumi na kutoa nafasi kwa familia nyingi kuinuka kimaendeleo.


Aidha amesema huduma ya Bolt imeongeza ushindani katika sekta ya usafiri wa mijini na kuleta ubora wa huduma pamoja na fursa mpya za kifedha kwa madereva katika mikoa mbalimbali ya nchi huku akisisitiza kwa kusema Bolt haijaja kutoa huduma pekee bali imekuja kujenga ajira endelevu na kuchangia pato la taifa kupitia teknolojia.


Kwa upande wake Mwanzilishi wa Chama cha Maofisa Uhusiano Tanzania Bwana Loti Makuza alisema mkutano huo umelenga kuongeza uelewa kwa maofisa uhusiano ili wawe tayari kuijenga imani kati ya serikali na wananchi.

No comments: